Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini anayemaliza
muda wake Mhe. Yahel Vilan.
Balozi huyo alikutana na Makamu wa
Rais na kumuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia nchini ulikuwa
umemalizika. akamu wa Rais alisema anafurahi kuona Idadi kubwa ya
Watalii kutoka Israel wanaokuja Tanzania.
“Tunawakaribisha sana Tanzania, waje kwa wingi wao, tunawakaribisha kwa mikono miwili” na alimuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili.
Kwa
upande wake Balozi Yahel alisema watalii kutoka nchini Israel
wameongezeka kutokana na kuvutiwa na mazingira mazuri , amani na utulivu
wa nchi.
Balozi Yahel alisema atakuwa mjumbe wa kuitangaza Tanzania popote duniani .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto)
ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu
wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kuaga .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) ambaye
muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa
Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kuaga .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan
(kushoto)ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga
Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam
kwa lengo la kuaga .
No comments:
Post a Comment