HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » Aveva, Kaburu kuendelea kusota rumande

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya inayowakabili vigogo wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu kuwa wanaendelea na uchunguzi na kwamba wamepeleka nyaraka kwa mtaalamu wa maandishi hivyo wanasubiri ripoti .
Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson amedai leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.
Wakili wa washitakiwa, Evodius Mtawala amedai mahakama ilipanga tarehe ya jana kwa ajili ya kusisitiza upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi hivyo wanaomba tarehe ya karibu. Hakimu Nongwa aliutaka upande wa mashitaka kujitahidi kupata ripoti hiyo kwa kuwa washitakiwa wako gerezani na kwamba wangekuwa nje wasingesumbuliwa sana.
Hata hivyo, ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 8 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kughushi na kutakatisha fedha. Inadaiwa Machi 15, mwaka jana, jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja walighushi fomu ya kuhamisha fedha kuonesha kwamba Klabu ya Simba inalipa deni la Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva, kitu ambacho si kweli.
Katika mashitaka ya pili yanayomkabili Aveva, inadaiwa Machi 15, mwaka jana maeneo ya Benki ya CRDB tawi la Azikiwe wilayani Ilala, Dar es Salaam, alitoa nyaraka hiyo ya uongo kwa benki hiyo kuonesha kuwa Klabu hiyo inalipa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva.
Pia inadaiwa tarehe tofauti tofauti kati ya Machi 15 na Juni 29, mwaka jana, ndani ya mkoa huo, washitakiwa walikula njama kutakatisha fedha Dola za Marekani 300,000 huku wakijua kwamba fedha hizo ni zao la uhalifu ambalo ni kughushi. Machi 15 mwaka jana, katika Benki ya Barclays Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Aveva alijipatia Dola za Marekani 300,000 wakati akijua kuwa alipata fedha hizo kutokana na nyaraka za kughushi.
Katika mashitaka ya tano yanayomkabili Nyange, ilidaiwa Machi 15, mwaka jana katika tawi la Barclays tawi la Mikocheni, alimsaidia Aveva kupata fedha kutoka katika benki hiyo huku akijua kwamba ni zao la uhalifu ambalo ni kutokana na kughushi fomu ya kuhamishia fedha. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: