Ama hakika wazee wetu wa zamani waliosema “Muonja asali haonji mara moja” hawakukosea! kwani msemo huo unakamilika ambapo dunia ya sasa wanandoa au watu walio kwenye mahusiano wanaongoza kuchepuka hii sio tu kwa sababu ya utandawazi bali ukweli ni kwamba usaliti ni ‘addiction’ kama walivyowatumiaji wa sigara na madawa ya kulevya hivyo kuacha ni kazi ngumu sana, huo sio mtazamo wangu bali ni kutoka kwa watafiti.
Kwa mujibu wa ripoti ya tafiti iliyofanywa na jarida la Nature Neuroscience zinaonesha kuwa watu waliowahi kuwasaliti wenza wao kwenye mahusiano kamwe hawataacha tabia hiyo mpaka mwisho wa mahusiano yao.
Utafiti huo unaonesha kuwa Mwanaume/Mwanamke akishachepuka ubongo hujenga tabia ya kudanganya na kuanza kuongeza tamaa ya kutokuridhika hivyo hata kama akiwa kwenye Ndoa/Mahusiano ya kawaida ni ngumu kubaki mtu mmoja.
Hata hivyo utafiti huo umeonesha Msaliti hata kama akikamatwa na mwenza wake mara kadhaa hujutia tu kwa muda lakini baadae hurudia tabia hiyo ni kutokana na ubongo mwenendo wa ubongo na mara nyingi muhusika hutumia akili nyingi kumdanganya mwenzie.
Utafiti huo uliohusisha wanandoa 2,800 waliowahi kuchepuka kwenye ndoa zao kutoka barani Ulaya, Amerika Kaskazini na Afrika na umeonesha asilimia 89% ya wanandoa waliowahi kuchepuka kwenye ndoa zao wamekiri bado wanaendelea na mchezo huo kwa siri huku asilimia 10% wakisema wanatamani ila wanawaheshimu wenzawao huku asilimia 1% ndiyo wamesema wameacha mchezo huo.
“Sababu za utafiti wetu ni kutokana na ongezeko la wanandoa kusalitiana kwenye mahusiano na utafiti wetu umeonesha ni hisia tu ndiyo zinapelekea tatizo hilo, na wasilaumiwe tu wahusika hii huathiri ubongo kwa kiasi fulani tumeona wanandoa wengi wanaofanya hivyo huwa wanausiri mkubwa na uongo uliokithiri bila shaka baada ya tafiti huu wanandoa kuna vitu watakuwa wamejifunza.“amesema moja ya waandaaji wa utafiti huo, Neil Garrett kwenye mahojiano yake na jarida la afya la Elite Daily.
Hata hivyo, utafiti huo umeonesha wanaume ndio wenye hisia kali kuliko wanawake linapotokea suala la matamanio.
No comments:
Post a Comment