KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali
(TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kesho Ijumaa (Agosti 11, 2017)wameandaa kipindi maalum kwa wagombea Urais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kitakachofanyika mjini Dodoma kuanzia majira ya
saa 3 usiku.
Kipindi hicho maalumu kitarushwa mubashara kupitia TBC pamoja
na ‘TSN Online’ kitawakutanisha wagombea urais; Ally Mayay, Fredrick Mwakalebela,
Wallece Karia, Shija Richard, Iman Madega na Emmanuel Kimbe ikiwa ni saa chache
kabla ya siku ya uchaguzi yaani kesho kutwa Jumamosi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya kipindi hicho, Enock Bwigane alisema kuwa ili mpira
wa miguu uendelee kukua nchini TBC na TSN iliona ni vyema ikawakutanisha
wagombea kwenye jukwaa moja ili waweze kuwaambia wananchi ni kwa njia gani
wataweza kuinua soka la Tanzania kama wakipewa dhamana hiyo.
Alisema,
“Kuna takribani wapiga kura 130, wagombea urais ni sita lakini mmoja ndiye
atakayeshinda na kuongoza shirikisho hilo kwa miaka minne kabla ya uchaguzi
mwingine hivyo tumeona haja ya kuwakutanisha na kuwawezesha wananchi waweze
kuwafahamu...
“…Naamini
fursa ya kuwakutanisha na kuwapa nafasi ya kuwaeleza watanzania sera na mipango
yao ya kuboresha soka ni jambo la msingi na ni haki yao ukizingatia kuwa leo
ndiyo siku ya mwisho ya kampeni,” alisema Bwigane.
Naye Katibu
wa kamati hiyo, Alfred Lasteck alisema kuwa TSN ikishirikiana na TBC inatambua
nini watanzania wanataka kufahamu kuhusu mpira wa miguu na ndiyo maana imepanga
kuwakutanisha wagombea ili waweze kuzungumza na umma kabla ya uchaguzi hapo
kesho.
“Kuna zaidi ya Watanzania milioni 50 ambao
wangependa kufahamu ni nini kitasaidia soka la Tanzania ili liweze kuendelea
kutoka lilipo sasa hadi kufikia mafanikio.
“Hivyo ni
nafasi ya kipekee kwa kila mtanzania kufuatilia matangazo mubashara yatakayorushwa
na TBC1 pamoja na TSN Online kipindi kile ambacho wagombea wote wa Urais watakapokuwa
wakielezea mipango yao kuhusu mpira wa miguu nchini,” alisema Lasteck.
No comments:
Post a Comment