Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ameiagiza timu ya uendeshaji wa huduma za afya ya mkoa wa Rukwa, kusimamia utendaji wa vituo vyote vya kutolea huduma ya afya ili kudhibiti takwimu zisizokuwa sahihi, ambazo zinasababisha bajeti ya dawa isiwe halisi na kuendelea kuwepo upungufu mkubwa wa dawa.
Waziri huyo Ummy Mwalimu akiongea kwenye kituo cha afya cha Matai wilayani Kalambo, ameshangazwa kuona menejimenti ya kituo hicho cha afya ambacho hivi sasa kinatumika kama hospitali ya wilaya hiyo, inakuwa haijui kwa uhalisi bajeti ya dawa, na huku wakiendelea kupata bajeti ya kiwango cha kata kwa idadi ya watu elfu tatu, wakati sasa matai ni makao makuu ya wilaya na idadi ya watu ni zaidi ya 10,000 jambo ambalo haliendani na upatikanaji wa dawa.
Nao baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo akiwemo katibu tawala Bw. Frank Sichalwe, wamemueleza waziri huyo wa afya kuhusu utendaji wa bohari kuu ya dawa MSD kanda ya Mbeya, kuwa mara nyingi wamekuwa wakileta dawa nyingi ambazo tayari zinakaribia kuisha muda wa matumizi, na kwamba wilaya inakabiliwa na tatizo kubwa la kutokuwa na gari la wagonjwa kabisa.
Waziri Ummy Mwalimu akimuuliza mmoja wa mama aliyefika kupata matibabu ya nje kwenye kituo cha afya cha Mazwi kama amefika muda mrefu na hajapata matibabu, waziri huyo yupo mkoani Rukwa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kukagua huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo vya huduma nchini.
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na mama mjamzito aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa.Waziri Ummy alisisitiza watoa huduma kuhakikisha awatoa huduma wa afya wanajitahidi kuepusha vifo vianavyoweka kuepukika kutokana na uzazi
Waziri wa Afya akiongea na akina mama wajawazito waliolazwa kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa
Waziri akimjulia hali mama mjamzito aliyelezwa kwenye kituo cha afya katika manispaa ya Sumbawanga.
Moja ya kipaumbele cha wizara ya afya katika kuokoa vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua ni Damu Salama, Waziri wa Afya akiangalia akikagua benki ya damu salama iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa.
Baadhi ya watumishi wa sekta ya afya wa manispaa na mkoa wa Rukwa wakimsikiliza waziri wa afya(hayupo pichani) wakati wa kuongea na watumishi hao ambao walitoa changamoto zao zinazowakabili katika utendaji kazi zao za kila siku
Mmoja wa watumishi wa kada ya afya akiulizwa swali wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara ya waziri huyo. Waziri wa afya yupo mkoani Rukwa kikazi ambapo aliweza kutembelea vituo vya afya na hospitali zilizopo wilaya za Nkasi, Kalambo, Manispaa ya Sumbawanga na hospitali ya Mkoa ya Rukwa(picha zote na Wizara ya afya)
No comments:
Post a Comment