Kansa ni ugonjwa unaotokea katika viini vya mwili vinavyohusika na kurithisha tabia kutoka kizazi kimoja hadi kingine (genes) – ni ugonjwa unaotokana kwa kubadilika kwa genes zinazohusika na ufanyaji kazi wa seli za mwili, na hasa zile zinazohusika na namna seli zinavyokua na kujigawa.
Mabadiliko katika genes yanaweza kuwa ya kurithi kutoka kwa wazazi au yanaweza kutokea katika kipindi cha maisha ya mtu kutokana na hitilafu zilizotokea wakati wa kugawanyika kwa seli au kutokana na uharibifu wa DNA uliotokana na vitu vilivyopo kwenye mazingira viitwavyo carcinogens. Vitu vya kwenye mazingira vinavyosaidia kuharibu DNA na kukua kwa kansa (carcinogens) ni kama kemikali zilizopo ndani ya moshi wa tumbaku, asbestos, arsenic, mionzi ya gamma, X-rays, moshi wa magari na mionzi ya jua (UV rays).
Umri wa mtu unapokuwa mkubwa uwezekano wa kutokea dosari katika mabadiliko ya DNA yanayosababisha kansa huongezeka na kufanya umri kuwa ni sababu moja ya kuweza kupata kansa kirahisi. Kuna virusi wanaohusishwa na kansa kama human papillomavirus (wanaosababisha kansa ya cervics ), hepatitis B na C (wanaosababisha kansa ya ini), Epstein-Barr virus (anayesababisha baadhi ya kansa za utotoni), Human immunodeficiency virus (HIV) -na kitu cho chote kinachodhoofisha kinga za mwili.
Kila mtu mwenye saratani ana mmchanganyiko tofauti wa sababu zilizopelekea kutokea mabadiliko hayo katika genes zake. Kansa inavyozidi kukua, mabadiliko za ziada huongezeka. Uvimbe mmoja unaweza kuwa na seli zilizozalishwa kutokana na aina tofauti ya badiliko katika genes.
Kansa iliyoenea kutoka sehemu moja ya mwili ilipoanzia hadi sehemu nyingine huitwa metastatic cancer na tendo la kansa kuenea kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine ya mwili huitwa metastasis. Kansa iliyoenea kutoka sehemu moja ya mwili hadi sehemu nyingine huwa na aina ya seli zilezile za sehemu ambako ilitokea na hupewa jina lile lile la aina ya kansa ya sehemu ya mwanzo ilikotokea. Kwa mfano, kansa ya ziwa iliyoenea na kwenda kujenga uvimbe katika mapafu haitaitwa kansa ya mapafu bali metastatic cancer ya ziwa na uchunguzi kwa vyombo maalumu wa seli za sehemu hizi mbili utaonyesha kufanana kwa seli za sehemu hizo mbili toauti. Kansa hizi zinazotokea kwa kuenea kutoka sehemu moja ya mwili hadi nyingine (metastatic cancers) huleta madhara makubwa kwa ufanyaji kazi wa mwili na idadi kubwa ya watu
wanaofariki kwa saratani, hufariki kwa sababu ya aina hii ya kansa.
Aina Za Kansa
Mara nyingi aina za kansa hutajwa kutokana na kiungo ambako kansa hiyo ilianzia. Kwa mfano, kansa iliyoanzia kwenye mapafu itaitwa kansa ya mapafu na ile iliyoanzaia kwenye ubongo itaitwa kansa ya ubongo. Kuna namna nyingine za kuzitofautisha kansa, kama vile kwa kutaja aina ya seli zilizozijenga kansa hizo.
Hapa chini ni baadhi ya makundi ya kansa zilizoanzia kwenye aina fulani ya seli:
Carcinoma
Carcinomas ndizo kansa zinazoshambulia zaidi watu kuliko aina nyingine zote za kansa. Kansa hizi zinajengwa na seli zinazofunika maeneo ya ndani na ya nje ya mwili (epithelial cells) ambazo zipo za
aina nyingi.
Carcinoma hupewa majina kutokana na aina ya seli zilipoanzia:
Adenocarcinoma ni kansa zinajojenga seli za epithelial zinazozalisha majimaji au ute. Kansa nyingi za maziwa, utumbo na tezi kuu huwa ni za aina hii (adenocarcinomas).
Basal cell carcinoma ni aina ya kansa inayoanzia kwenye tabaka la chini la epidermis – epidermis ni sehemu ya juu ya ngozi ya mwili.
Squamous cell carcinoma ni kansa inayojenga kwenye seli ziitwazo squamous cells – ambazo ni seli za epithelial zilizo chini ya ngozi mara baada ya sehemu ya juu kabisa ya ngozi. seli za Squamous pia hufunika viungo vingine vingi vya mwili ikiwa ni pamoja na tumbo, utumbo, mapafu, kibofu cha mkojo na figo. Kansa za aina hii pia huitwa epidermoid carcinomas.
Pia kuna aina ya kansa iitwayo Transitional cell carcinoma ambayo hushambulia ngozi inayofunika kibofu cha mkojo, ureters, sehemu za figo na maeneo mengine.
Sarcoma
Kundi hili la kansa linajumuisha saratani zinazojenga kwenye mifupa na sehemu laini za amwili kama kwenye misuli, mafuta, mishipa ya damu. mishipa ya lymph, tendons na ligaments.
Katika kansa za mifupa osteosarcoma ndiyo inayoshambulia idadi kubwa zaidi ya watu. Osteosarcoma huanzia kwenye seli za kuzalisha mifupa mipya (osteoblasts) na ni aina saratani amabya hushambulia zaidi vijana wa umri mdogo. Saratani hii mara nyngi hujenga sehemu inapoishia mifupa mirefu ya mwili ambayo ni mifupa ya mikono na miguu. Kwa watoto wachanga na wale wa umri wa zaidi ya miaka kumi, hujenga zaidi karibu na magoti.
Dalili kuu za osteosarcoma ni uvimbe kwenye eneo la mfupa, maumivu kwenye mfupa au joint na kuvunjika kwa mfupa kusikoambatana na sababu yo yote ile. Kansa hii huchochewa na tiba ya mionzi na matumizi ya vidonge vya kuzuia kansa vinavyoitwa alkylating agents.
Aina nyingine ya kansa ya mifupa inaitwa Ewing sarcoma.
Aina za kansa zinazoshambulia viungo laini vya mwili ni leiomyosarcoma, Kaposi’s sarcoma, malignant fibrous histiocytoma, liposarcoma na dermatofibrosarcoma protuberans.
Kaposi sarcoma au kaposi’s sarcoma ni aina ya kansa inayojenga au kuleta mabadiliko kwenye viungo vya ngozi, utando laini wa kwenye midomo, pua na koo na maeneo mengine ya mwili.
Leukemia
Hizi ni kansa zinazoanzia kwenye sehemu za uzalishaji wa chembechembe za damu zilizopo ndani ya mifupa
(bone marrow). Kansa hizi hazijengi uvimbe wa namna yo yote bali huongeza idadi kubwa ya chembechembe nyeupe za damu zilizo za kipekee katika damu na katika eneo la uzalishaji wa chembechembe za damu (bone marrow) na kuzizidi kabisa chembechembe nyekundu za damu kiidadi. Hali hii ikitokea mwili hushindwa
kupata kiwango cha hewa ya oksijeni kinachotakiwa ili viungo vyake vifanya kazi vizuri, hushindwa kudhibiti utokwaji wa damu mwilini na kupambana na maambukizi.
Leukemia ni kansa inayowapata zaidi watu wenye umri wa zaidi ya miaka 55 na watoto wadogo chini ya miaka 15 na mara nyingi hutibiwa kwa chemotherapy.
Lymphoma
Lymphoma ni kansa inayoanzia kwenye Tcells au B cells au kwa neno jingine lymphocytes ambazo ni seli nyeupe za kupambana na magonjwa – ni sehemu ya kinga za mwili. Saratani hii inapotokea, seli hizi zisizo za kawaida hujijenga kwenye mishipa ya lymph na sehemu nyingine za mwili.
Kuna aina kuu mbili za lymphoma:
Hodgkin lymphoma – hizi huanzia kwenye B cells
Non-Hodgkin lymphoma – Hiki ni kikundi kikubwa cha kansa zinazoanzia kwenye lymphoctes. Kansa hizi hukua haraka sana au taratibu na zaweza kuanzia kwenye B cells au T cells.
Multiple Myeloma
Hii ni aina ya kansa inayoanzia kwenye seli za plasma, ambayo ni aina nyingine ya seli zinazohusika na kinga ya mwili. Seli hizi za kansa zisizo za kawaida (myeloma cells) hujengwa kwenye sehemu ya mifupa inayohusika na ujenzi wa seli za damu (bone marrow) na husababisha uvimbe kwenye mifupa yote ya mwili. Kansa ya aina hii pia huitwa plasma cell myeloma au ugonjwa wa Kahler.
Melanoma
Melanona ni aina ya kansa inayoanzia kwenye seli zinazojenga melanin – vitu vinavyoipa ngozi ya mwili rangi yake. Melanomas nyingi hujenga juu ya ngozi ya mwili lakini mara nyingine huweza kujenga kwenye sehemu tofauti ya mwili yenye rangi, kama kwenye macho.
-
No comments:
Post a Comment