Miguu kutoa harufu mbaya ni tatizo sugu linalowakabili baadhi ya watu katika jamii, wengi wakiwa wanaume.
Katika nyakati hizi za mvua, tatizo hili linaonekana kuzidi kuwa sugu, hali inayosababisha kuwepo na harufu mbaya hasa kwenye mikusanyiko ya watu kama vile kwenye daladala.
Lakini watu wengi wenye tatizo hili huwa wagumu kukubaliana na hali yao hata kutafuta tiba mahususi inaweza kuwaondolea kero hiyo.
Licha
ya kuwepo sababu mbalimbali zinazochangia kutokea hali hiyo, ukweli
utabaki kuwa uchafu ndiyo chanzo kikuu cha miguu kutoa harufu.
Kwa
kiasi kikubwa uchafu huo ndio unasababisha kuzaliwa kwa vijidudu
vinavyoleta harufu mbaya kwenye miguu na kuwakera wanaokumbana na harufu
hiyo.
Pamoja
na tiba nyingine za kitaalamu ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza
kupata, usafi ni jambo kubwa analopaswa kuzingatia zaidi hasa kipindi
hiki cha mvua.
Ukigundua una tatizo hili, hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara ukiiacha mikavu muda wote ili kuepusha unyevunyevu.
Kila unapovaa viatu vya kufunika, hakikisha unavaa soksi safi na kavu.
Epuka kurudia soksi au kuvaa ambazo hazijakauka vyema kwani zinaweza kusababisha miguu kunuka mara dufu.
Usivae
viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika
kwenye hewa ili vikauke kupunguza uwezekano wa kutokea harufu.
Kama
utahisi tatizo ni kubwa zaidi ni vyema utumie sabuni zenye dawa za kuua
vijidudu pamoja na mafuta maalumu yanayoweza kutumika miguuni.
Ikishindikana, nenda kwa wataalamu wa afya.
Chazo: Docta Joh Blog




No comments:
Post a Comment