HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » Serikali kufanya tathmini mahitaji mita za luku

Waziri wa Nishati, Dk Merdard Kalemani amesema Serikali itafanya tathmini ya mahitaji ya mita za luku kabla ya kupiga marufuku uagizaji mita hizo kutoka nje ya nchi.
Amesema tathmini hiyo itafanyika kwa siku 90 kuanzia leo Jumamosi Machi 24, 2018 baada ya hapo hakutakuwa na uagizaji wa mita hizo kutoka nje kutokana na uzalishaji ulioanza kupitia viwanda vya ndani.
Ametoa kauli hiyo leo Machi 24, 2018 wakati wa ziara katika kiwanda cha kutengeneza mita za umeme wa luku cha Baobab Energy System Tanzania (Best).
Kiwanda hicho kimeanza kutengeneza mita za aina hiyo Machi 15, 2018 kikianza na uzalishaji wa wastani wa mita hizo 1000 kwa siku zinazotumika kwa wateja wa kawaida.

Chanzo: Mwananchi

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: