na wengine wengi ambao wanaweza kuathirika na mazingira ya mahali pa kazi.
Usalama na afya mahala pa kazi inaweza
kuwa na umuhimu kwa sababu
ya maadili, kisheria, na kifedha.
Mashirika yote yana wajibu wa kuhudumia
ili kuhakikisha kwamba wafanyakazi na
mtu mwingine yeyote ambaye haathiriki na
kubaki salama wakati wote wa kazi.
Majukumu au sababu za kimaadili ni lazima
zihusishe ulinzi wa maisha
ya mfanyakazi na afya yake wakati wa
kazi.
Pia Sababu za kisheria zinazohusiana na kuzuia madhara, kwa kutoa adhabu na fidia ya sheria ya
kulinda usalama wa mfanyakazi
na afya yake.
Kitengo cha usalama mahala pa kazi, Pia kitahakikisha kinapunguza visababishi vya majeraha, kwa kuumia na pia kwa ugonjwa kwa kugharamia huduma za matibabu,
likizo ya ugonjwa na gharama ulemavu faida.
Kitengo cha usalama mahala pa kazi,kuinaweza kuhusisha mwingiliano na uhusiano
kati ya maeneo mengi ya kazi,
usafi wa kazi, afya ya umma, usalama uhandisi,
viwanda uhandisi, na saikolojia ya afya
kazini
Afya na usalma mahala
pa kazi ni jambo muhimu sana katika maendeleo ya kiwanda na
kwa mfanyakazi katika ufanisi wa kazi zake, pamoja na kutambua na kudhibiti hali ambayo inaweza kusababisha madhara
nakuadhiri afya kutokana na kazi
ambayo mtu anaifanya.
Afya na Usalama sehemu za kazi
ni jukumu letu wote. Je! Ni nini unafahamu kuhusu Afya na Usalama Sehemu za Kazi?
Je una wajibika kiasi gani kupunguza ajali sehemu yako ya kazi?
Je sheria za Tanzania
zinatoa msimamo gani juu ya Afya na Usalama Sehemu za Kazi (OSH)?
Tanzania ina sheria
kadhaa zinazosimamia masuala ya Afya na Usalama sehemu za kazi kwa wafanyakazi,
mojawapo ikiwa ni Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004. Vilevile
sheria mahususi na ya moja kwa moja ni sheria ya Afya na Usalama sehemu za kazi
ya mwaka 2003. Sheria hii inalenga kulinda haki za wafanyakazi kiafya na
kiusalama sehemu za kazi.
Vile vile sheria hii inalenga kulinda afya na usalama
wa mtu tofauti na mfanyakazi lakini alieko sehemu ya kazi ( kwa mfano mteja)
dhidi ya madhara ya kiafya na kiusalama yatokanayo na kazi za mtu alieko kazini
na kuweza kuunganisha mambo haya.
Je sheria ya Usalama
na Afya sehemu za Kazi ya mwaka 2003 inagusa sehemu gani?
Sheria hii inagusa
viwanda vyote na sehemu zote za kazi ambazo hazijapatiwa msamaha na Waziri kama
sheria inavyosema.
Je sheria imeweka
wajibu wa mfanyakazi?
Ndio, Zifuatazo ni
baadhi ya wajibu wa mfanyakazi uliowekwa na sheria:
- Wafanyakazi ni
lazima wachukue tahadhari za makusudi dhidi ya usalama na afya zao na mtu mwingine ambaye anaweza
kuathirika na vitendo vyao au kutokuepo kwako kazini.
- Vile vile
wafanyakazi wana wajibu wa kushirikiana na Waajiri ili kuwezesha mahitaji yaliyowekwa na Waajiri kufikiwa au
kuzingatiwa kwa usahihi.
- Wafanyakazi pia
wana wajibu wa kutekeleza amri yeyote kisheria walizopewa na zinazo heshimu
kanuni na taratibu za afya na usalama zilizowekwa na Waajiri au mtu mwenye
mamlaka kwa madhumuni ya kulinda afya na kuhakikisha usalama.
- Kutoa taarifa kwa
mwajiri au mwakilishi wa usalama na afya sehemu za kazi juu ya kuwepo kwa hali
isiyokuwa salama au yenye madhara kiafya inayojitokeza sehemu za kazi.
- Kutoa taarifa kwa mwajiri au mwakilishi wa usalama na afya sehemu za kazi juu ya hali yoyote au ajali ambayo inaweza kusababisha madhara kwa afya zao mapema iwezekanavyo ( sio zaidi ya mwisho wa zamu labda kama hali imepelekea hivyo)
Mwajiri ana wajibu
gani chini ya sheria hii?
Wajibu wa mwajiri
chini ya sheria ya Usalama na Afya sehemu za Kazi ni kama ifuatavyo:
Kusajili eneo lake
la kazi na Wakala wa Usalama na Afya sehemu za kazi
- Kupima afya za wafanyakazi mara kwa mara kwa kuzingatia sheria.
- Kuchagua mwakilishi wa usalama na afya sehemu za kazi katika sehemu yenye wafanyakazi wanne na zaidi.
- Mwajiri ni lazima ahakikishe mahali pa kazi ni salama kiafya na hatakiwi kuruhusu mfanyakazi kufanya kazi yenye madhara au hatarishi.
- Ni lazima wawape wafanyakazi taarifa juu ya hatari iliyopo katika eneo la kazi
- Ni lazima wahakikishe hatari imedhibitiwa hadi hatua ya chini kabisa kabla ya kutoa vifaa vya kujikinga.
- Ni lazima watoe nguo za kujikinga pale inapolazimu.
- Ni lazima watoe mafunzo kwa wafanyakazi wanaotumia mashine na vifaa hatarishi kuhakikisha wanafahamu hatua za kiusalama.
- Ni lazima wawazuie wafanyakazi kutumia au kufanya kazi na vitu au mashine hatarishi mpaka kanuni zote za usalama zifuatwe.
- Ni lazima ahakikishe kwamba mashine hatarishi zinafanya kazi vizuri na ziko salama kuzitumia.
- Ni lazima wahakikishe kuwa mashine hatarishi zina tahadhari au notisi kuonyesha kua ni hatari.
- Ni lazima wahakikishe kuwa mtu anyejua kazi anasimamia utendaji kazi kuhakikisha usalama wa wafanyakazi.
- Ni lazima waache sehemu za kazi wazi ili kuruhusu wafanyakazi kutoka inapotokea hatari.
Je kuna adhabu yoyote
pale ambapo mfanyakazi au mwajiri anakikiuka sheria?
Inapotokea ajali
iliyosababishwa na mwajiri na ikamuumiza au hata kumuua mfanyakazi basi mwajiri
atawajibika kulipa fidia isiyopungua milioni kumi (10) au kutumikia kifungo cha
kipindi kisichozidi miaka miwili(2) au kufungwa na kulipa fidia kwa pamoja.
Mahakama pia inaweza kuongeza juu ya fidia au badala ya fidia kutoa amri
kuondolewa kwa kilichosababisha tatizo.
Kama mfanyakazi
atavunja au ataenda kinyume na sheria ilivyosema basi atawajibika kulipa faini
au kufungwa au kupata vyote ( kifungo na faini) kutegemea na kosa lenyewe.
Je mwajiri anaweza
kumuadhibu mfanyakazi kwa kulalamikia hali ya usalama?
Hapana, sheria
inamkataza mwajiri kumfuta mtu kazi, kupunguza mshahara na marupurupu yake,
kubadilisha vigezo na masharti ya mkataba wa kazi kwa sababu zifuatazo:
• Kutoa ushahidi mahakamani kuhusu hali zao
za kazi.
• Kujibu maombi au maswali ya mkaguzi
• Kukataa kufanya chochote ambacho ni kinyume
na sheria
• Kutoa taarifa kuhusu hali zao za kazi
• Kutii vikwazo vya kisheria, mahitaji,
maombi au maelekezo yatolewayo na wakaguzi
• Kupata magonjwa yatokanayo na kazi na hata
yale mengine yasiyotokana na kazi
Je mwajiri anatakiwa
kutoa taarifa za ajali zitokeazo sehemu za kazi?
Mwajiri ana wajibu wa
kutoa taarifa juu ya tukio au ajali yoyote iliyotokea eneo la kazi na kupelekea
kifo, maumivu au majeraha ya mwili, kupoteza fahamu, magonjwa yatokanayo na
kazi au yamempa ulemavu wa moja kwa moja mfanyakazi, ndani ya saa 24 kutoka
tukio au ajali kutokea. Ndani ya siku saba kutoka tukio au ajali kutolewa
taarifa mwajiri anatakiwa kutuma taarifa kamili inayoelezea tukio au ajali
hiyo.
Ni namna gani
vipengele vya sheria hii vinasimamiwa na kuhakikisha vinatekelezwa?
Wakala wa Usalama na
Afya sehemu za kazi (OSHA) iliyoanzishwa chini ya sheria ya wakala wenye kutoa
maamuzi Na. 30 ya mwaka 1997 ndio wasimamizi wa sheria Na. 5 ya usalama na afya
sehemu za kazi ya mwaka 2003
Malengo ya msingi ya
Wakala wa usalama na afya sehemu za kazi (OSHA) ni kuhakikisha kuanzishwa na
kuendelea kuwepo na mazingira salama ya kazi ambayo ni huru dhidi ya madhara
yatokanayo na kazi amabyo yanweza kupelekea kuumia au magonjwa kwa wafanyakazi
katika eneo la kazi. Wakala wameajiri wakaguzi wa kazi ambao moja ya wajibu wao
ni ukaguzi wa afya na usalama sehemu za kazi. Baada ya kuandaa ripoti,
hupelekwa kwa mkaguzi mkuu kwa ajili ya kuchukua hatua ambazo zinaweza kua:
• Kumshauri mwajiri ipasavyo.
• Kutoa notisi ya kuboresha hali.
• Kutoa notisi ya kuzuia.
• Kupeleka suala mahakamani.
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
No comments:
Post a Comment