HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » Kombe la Europa lililokuwa limeibwa, lapatikana nchini Mexico

Kombe la ligi ya Europa lililokuwa limeibwa baada ya kuwekwa hadharani nchini Mexico, limepatikana saa kadhaa baadaye, kwa mujibu wa Mamlaka za Jimbo la Guanajuato , leo Jumamosi.

Kombe hilo lilitolewa mbele ya umati wa mashabiki wa mpira wa miguu katika uwanja wa mji wa Leon jana usiku, lilichukuliwa muda mfupi kutoka ndani ya gari baada ya tukio hilo.

“Tumefanikiwa kulipata kombe baada ya kupokea taarifa za kuwa limeibwa wakati likiwa linasafirishwa ,” imeweka wazi akaunti ya Twitter ya mwendesha mashtaka wa Umma wa Jimbo la Guanajuato, huku akiambatanisha na picha ya kombe hilo.


Hakuna taarifa zaidi imetolewa kuhusu nani alilichukua Kombe hilo, na wapi lilipatikana na iwapo kuna yeyote aliyekamatwa.

Tukio la kuweka hadharani Kombe hilo liliratibiwa na moja ya Bodi inayodhaminiwa na UEFA ya kusimamia Soka Ulaya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: