HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » Rais Magufuli kuzindua Nyumba za Polisi Arusha, April 7

Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia kinachotarajiwa kuzinduliwa April 7 Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya Nyumba za Polisi zinazotarajiwa kuzinduliwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli

Na Vero Ignatus, Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pohn Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi na vituo vya polisi Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wahabari Kamanda wa polisi jijini hapa DCP Charles Mkumbo amesema kuwa kutakuwa na uzinduzi wa vituo viwili cha Utalii na Diplomasia na kingine ni Kituo cha daraja la kati kilichopo Murieti Jijini Arusha. 
Kamanda Mkumbo amesema kuwa kutakuwepo pia na maonyesho mbalimbali ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi za kuwahudumia wananchi ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid . 

Amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwani hali ya usalama Jijini hapa umeimarishwa na amewaomba wajitokeze kwa wingi katika sherehe hizo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: