Ugonjwa wa Genital Warts ni hali ya kuota vinyama kwenye ngozi au utando
laini unaozunguka maeneo ya siri, ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya
kujamiiana (sexually transmitted infection kifupi STI).
Ugonjwa huu
unaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), shingo ya
kizazi (cervix) au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.
Ugonjwa
huu husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa kitaalamu Human Papilloma
Virus (HPV) ambavyo vipo zaidi ya aina 70 tofauti ingawa si wote
wanaosababisha maradhi haya ya maeneo ya siri.
Baadhi ya aina
nyingine za HPV husababisha kutokwa na vinyama kwenye ngozi inayozunguka
sehemu nyingine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu.
Baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya
kizazi kitaalamu huitwa Carcinoma of the cervix kwa wanawake au saratani
ya njia ya haja kubwa, kwa jinsia zote mbili.
Ugonjwa huu wa kuota
vinyama sehemu nyeti umejitokeza kwa kasi kubwa na watu wengi waliopatwa
na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile.
Kwa upande wa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka
maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi (cervics) bila
dalili kujitokeza.
Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa
kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha
njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni.
Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi
miezi 6 kwa ugonjwa wa kuota vinyama kujitokeza wazi, ingawa baadhi ya
wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yoyote
ile.
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
No comments:
Post a Comment