Mpenzi
msomaji, katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke huweza kupata
ujauzito feki, na ujauzito feki au kwa kitaalamu hujulikana kama Phantom, Pseudocyesis or False pregnancy,
ni hali inayompata mwanamke na kumfanya ajione ni mjamzito huku akipata
dalili zote za kumuaminisha kuwa yeye ni mjamzito wakati katika hali
halisi, yeye siyo mjamzito.
Miongoni mwa matatizo ambayo huweza kumfanya mwanamke apate tatizo hili ni pamoja na, matatizo ya kisaikolojia ambapo, mwanamke huwa na hofu sana ya kupata ujauzito na hivyo kumfanya wakati wote ahisi kuwa amepata ujauzito, hii huweza kumfanya apate tatizo hili.
Matatizo ya uvimbe tumboni, mwanamke anapokuwa na uvimbe tumboni na hasa katika mirija ya uzazi huweza kumfanya apate tatizo hili kwani uvimbe husababisha mirija ya uzazi ifunge na hivyo mwanamke kushindwa kuona siku zake, na kwa kuwa hataona siku zake basi kitu atakachofikiria ni ujauzito. Jambo lingine ni matatizo ya homoni ambayo huweza kumfanya mwanamke apate dalili hizi za ujauzito na akaamini kuwa yeye ni mjamzito na kumbe siyo sahihi.
Kutokana
na mapinduzi ya kitekinolojia katika sekta ya afya, matatizo haya
huweza kugundulika kwa kutumia vifaa na vipimo mbalimbali
vinavyopatikana katika hospitali na sehemu za kutolea huduma za afya.
Ikiwa kama changamoto katika afya za uzazi, ni vyema wanawake wakafika mapema katika sehemu za kutolea huduma za afya pindi wanapogundua au kuhisi kuwa ni wajawazito ili matatizo kama haya yaweze kugundulika mapema na kupata ushauri au huduma zinazostahili.
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
No comments:
Post a Comment