Baadhi ya vijana wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Mbinga wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu Kassian Nyandindi aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira na mmiliki wa Blogy ya Nyandind Gwiji la Matukio ambaye alifariki tarehe 10 na kuzikwa tarehe 12 katika makaburi ya Misheni Mjini Mbinga.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye aliyevaa shati la kitenge na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilayani humo Beda Hyera wakiweka udongo jana, katika kaburi la aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira kituo cha Mbinga Marehemu Kassina Nyandindi ambaye alizikwa katika makaburi ya Misheni Mbinga mjini.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari wa mkoa wa Ruvuma,wakiwa katika msiba wa mwandishi wa Habari wa Gazetila Majira kituo cha Mbinga wakati wa Ibada iliyofanyika numbani kwa marehemu Mtaa wa Ruhuwiko Mbinga mjini.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Beda Hyera akitoa salamu za Chama hicho katika msiba wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira wilaya ya Mbinga Marehemu Kassian Nyandindi aliyezikwa jana katika makaburi ya Misheni Mjini Mbinga.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye, akiongea na ndugu,jamaa,marafiki na waombolezaji waliofika katika msiba wa Marehemu Kassian Nyandindi ambaye alikuwa mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira aliyezikwa jana katika makaburi ya Misheni Mjini Mbinga.
Mama Mzazi wa maraehemu Kassian Nyandind Mwalimu Nyandindi akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake maraehemu Kassian Nyandindi ambaye alifariki Dunia kufuatia ajali ya pikipiki iliyotokea tarehe 9 katika eneo la Ruhuwiko Mbinga Mjini na kufariki Dunia katika hospitali ya Rufaa Songea tarehe 10 alipo pelekwa kwa ajili ya Matibabu na kufariki na kuzikwa tarehe 12 katika makaburi ya misheni Mbinga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Shafi Mpenda kushoto na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Gombo Samandito wakitoa heshima zao katika kaburi la aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira marehemu Kassian Nyandindi aliyefariki tarehe 10 na kuzikwa terehe 12 katika makaburi ya Misheni Mbinga mjini.
PICHA ZOTE NA MUHIDIN AMRI(MBINGA)
No comments:
Post a Comment