WADAU WA HUDUMA ZA UONGOZAJI NDEGE NCHINI WAKUTANA KUJADILI MABORESHO YA UTOAJI WA HUDUMA HIYO MUHIMU

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete akizungumza na wadau mbalimbaliwa usafiri wa Anga wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa huduma za uongozaji ndege uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Daniel Malanga akizungumza kuhusu namna wanavyosimamia masuala yote ya usafiri wa anga wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa wadau wa huduma za uongozaji ndege unaofanyika kwa siku mbili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi. Flora Alphonce akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa huduma za uongozaji ndege uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete(watatu kulia) akiwakabidhi vyeti baadhi ya wadhamini wa mkutano wa wadau wa huduma za Uongozaji ndege uanofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 12 hadi 13 Juni , 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau huduma za Uongozaji ndege wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa wadau uliofunguliwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau huduma za Uongozaji ndege mara baada ya kufungua mkutano wa wadau hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amefungua mkutano wa wadau wa huduma za uongozaji ndege nchini uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mhe. Mwakibete ameipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kwa kuandaa mkutano huu unaowaleta pamoja wadau wote muhimu wa huduma za uongozaji ndege ambapo kwa pamoja wanajadili na kuja na maazimio yatakayoboresha utoaji wa huduma hiyo.

"Nimefarijika sana kuwaona ninyi ambao ndio wadau wa huduma hii yenye upekee wake maana hapa imewaona marubani, waongozaji ndege, wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege, watoa taarifa za usalama wa anga, Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja nanyi kampuni za ndege. Hii ni ishara njema kwetu kama serikali kuwa mnayo nia moja ya kuhakikisha anga letu linahudumia kisasa na kwa umoja, hivyo serikali ipo nanyi katika masuala yote mtakayojadiliana kwenye mkutano huu”. amesema Mhe. Mwakibete

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Daniel Malanga aliwakaribisha wageni waalikwa kutoka nje ya Tanzania ambao wamekubali na kuitikia wito wa kuja kuhudhuria mkutano huu na kuwasihi kuwa huru katika kubadilishana uzoefu na ujuzi kwani huduma za Uongozaji Ndege zinategemeana.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa TCAA Flora Mwanshinga amesema mkutano huu unawaleta wadau wa huduma za uongozaji ndege nchini ili kujadili changamoto, maboresho, teknolojia mpya kwa lengo la kuboresha utendaji wa kila mdau anayetoa huduma.

Mkutano huo wa siku mbili ni sehemu ya jitihada za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania katika kuhakikisha huduma za uongozaji ndege zinazidi kuboreshwa ili kuendelea kuhudumia wadau wa sekta kwa ubora wenye  viwango vya kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.