TANZANIA NA CHINA YASHIRIKI MASHINDANO YA KIRAFIKI YA MPIRA WA MEZA KOMBE LA KIRAFIKI





BALOZI Wa China nchini Tanzania amehaidi kushikamana na watanzania kuhakikisha nchi hizo mbili zinabadilishana Utamaduni na kukuza sekta mbalimbali kwa lengo la kuongeza kipato .

Akizungumza na Wanahabari Leo Septemba 16,2023 Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian mara baada ya Kufungua Mashindano ya Kirafiki ya mpira wa Meza (tennis) Kombe la kirafiki mwaka 2023, ameeleza kuwa nchi ya china imekua ikishirikiana kwa karibu zaidi katika nyanja mbalimbali na nchi ya Tanzania kwa zaidi ya Miaka 60.

Aidha, Balozi amesema kupitia Mashindano hayo ya mpira wa meza (tennis) unalenga hasa kuendeleza undugu uliopo na mashirikiano mbalimbali pia Kuupa nafasi mchezo wa tennis kama michezo mengine hasa katika nchi ya Tanzania na kuhakikisha Afya zina imarika kwa washiriki wote baina ya nchi hizo mbili.

Pia amesema nchi ya china itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania ili kuvumbua fursa mbalimbali za kiuchumi,michezo na biashara.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la michezo taifa (BMT) Neema Msitha amesema kuwepo kwa Michezo baina ya nchi mbili tofauti ni mojawapo ya fursa mbili za kuonesha Michezo ina nafasi kubwa katika jamii.

"Shindano la mpira wa Meza (tennis) utaenda kukutanisha washiriki wa nchi hizo mbili yani China na Tanzania ambapo kila mtu atajifunza tamaduni ya mwenzake."

Hata hivyo ameomba Ubalozi wa China kusaidia mchezo huo kuingia Mashuleni ili watoto waweze kujifunza nakuupenda mchezo huo ili vipaji vipya vichanga viweze kuzalishwa kwa wingi.

Nae Afisa Utalii mkuu wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Alistidia Karaze amesema Nchi ya Tanzania na china zimekuwa na mahusiano mazuri kiuchumi na kidiplomasia kwa muda mrefu .

Hivyo kupitia ushirikiano huu wa Mashindano haya Kombe la taifa tutaongeza watalii wengi kwa mwaka 2023 ambapo tunatarajia kurejea kwenye takwimu za kabla ya janga la uviko_19.

Aidha Karaze ameongeza kuwa kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya mlipuko wa janga la Uviko_19 ,idadi ya watalii kutoka China iliongezeka kutoka watalii 25,444 mwaka 2015 hadi kufikia watalii 33,541 mwaka 2019 Sawa na ongezeko la asilimia 32.

Pia ameele namna bodi hiyo imekuwa ikibuni mikakati mbalimbali yenye lengo la kuongeza idadi ya watalii na uwekezaji kutoka nchini china.

" napenda kuwashukuru Ubalozi wa China kwa kuwa tayari muda wote kushirikiana nasi katika kuona namna ya kutekeleza mikakati hiyo ambapo kwa sasa inalenga kuboresha huduma zitolewazo kwa watalii kutoka China kuja Tanzania."
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akiwa na Katibu mtendaji wa Baraza la michezo taifa (BMT) Neema Msitha pamoja na wachezaji wa mchezo wa mpira wa Meza (table tennis) kombe la kirafiki 2023 kati ya nchi ya Tanzania na china ambayo yanalenga kuimarisha mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akizungumza na Wanahabari Leo Septemba 16,2023 katika ukumbi wa Diamond Jubilee katika ufunguzi wa Mashindano ya Kirafiki ya mpira wa Meza (table tennis) Kombe la kirafiki 2023 kati ya nchi ya china na Tanzania


No comments

Powered by Blogger.