HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » NAIBU WAZIRI MKUU AONGOZA MBIO ZA UDSM MARATHON, TCAA YASHIRIKI

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imetumia Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) kushiriki katika mbio za Marathon zilizoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mbio hizo zilizoongozwa na Mhe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, zilihudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Jakaya Kikwete .

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) ambayo kilele chake ni Desemba 7,2024. Maadhimisho ya mwaka huu pia inatimia miaka 80 tangu siku hii ilipoanza kuadhimishwa mnamo Desemba 7 mwaka 1944.

Watumishi wa TCAA licha ya kufanya kazi zao za ki udhibiti na kuongoza ndege pia hushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni hatua ya kuweka afya katika hali bora wakati wote.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameongoza mbio za UDSM Marathon za Chuo Kikuu cha Dar es salaam akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salama Kikwete ambaye ni mbunge wa Mchinga pamoja na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam








Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wakiwa kwenye Matembezi na Mbio zilijulikanazo kama UDSM Marathon











Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA wakiwa kwenye picha ya pamoja

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: