HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA TASWE YAANZA KWA KISHINDO UKUMBI WA CARDINAL RUGAMBWA OYSTERBAY - DAR

Maonyesho ya Kimataifa ya Ushirika wa akinamama wajasiliamali wa Tanzania (TASWE) yameanza kwa kishindo leo katika ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oysterbay. Akizungumza kwa juu ya maonyesho hayo, mwenyekiti na mwanzilishi wa Taswe Saccos, Bi Anna Matinde alisema "Maonyesho haya yamekuwa na hamasa kubwa wafanyabiashara na bidhaa kutoka Comorro, Afrika Mashariki na mikoa mbalimbali nchi zinapatikana hapa kwa wingi na kwa bei nafuu. "Tunawakaribisha wote mje mkutane na wafanyabiashara hawa pamoja na wadau wetu na kujionea bidhaa mbalimbali. Maonyesho yanaaza saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku", . Aliongeza Anna Matinde.
Mfanyabiashara kutoka Comorro, Siti Marahaba akiuza baadhi ya bidhaa zake katika maonyesho ya kimataifa ya Taswe
 Bi Sarah Abiudi akionyesha bidhaa za kiafrika zinazopatika katika maonyesho ya Taswe.
 Bi. Arafa Awadhi Mfanyabiasha mwanachama wa Taswe (kulia) akitoa maelezo juu ya bidhaa zake na mmoja ya mteja aliyetembelea maonyesho hayo
 Wafanyabiashara kutoka zanzibar wakionyesha bidhaa mbalimbali za kiasili zinazopatikana katika maonyesho ya kimataifa ya TASWE
 Mjasiliamali kutoka Nairobi Kenya, Bi Jesca Alphonce akionyesha namna ya ktumia moja kati ya bidhaa za urembo kwa wateja waliojitokeza kwenye maonyesho hayo
 Mfanyabiasha na mwanachama wa Taswe bi. Elizabeth akionyesha bidhaaa kwa wateja waliotembelea maonyesho
 Maonyesho haya ya akina mama wanachama wa Taswe yanaendelea ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oysterbay ambapo yalifunguliwa jana Machi 25, 2017 na kilele chake kitakuwa 31.03.2017.

SKULI YA KIJINI NA MBUYU TENDEE MATEMWE WAFAIDIKA NA MRADI WA UJENZI WA KIJIJI CHA UTALII CHA PENNYROYAL KWA KUTOA ELIMU YA AFYA NA MAZINGIRA

Maafisa Afya na Mazingira kutoka (SUZA) Nahya Khamis Nassor Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo cha SUZA ametoa mafunzo ya Afya na mazingira kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kijini Matemwe akizungumza na waandishi wa habari kufanikiwa kwa zoezi hilo la kutowa elimu kwa wanafunzi wa Skuli hiyo jinsi ya kuhifadhi mazingira na afya yao. Mradi huo unaosimamiwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Kitalii Matemwe Pennyroyal kwa kutowa elimu hiyo.
Amesema umeleta mafanikio makubwa kwa watoto hao jinsi ya kujilinda na maradhi ya mripuko kwa kupata elimu hiyo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa SUZA Nahya Khamis Nossor akitoa mafunzo ya Afya ya Mazingira kwa Wanafunzo wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe jinsi ya kujikinga na maradhi ya mripuko kwa kutunza mazingira safi katika maeneo yao na skuli, Mradi huo wa Elimu hiyo unafadhiliwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Matemwe  Pennyroyal.  
Wanafunzo wa Skuli ya Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakifuatila mafunzo hayo wakiwa katika darasa wakifuatilia kwa utulivu  wakiangalia vipeperushi vinavyoelezea utungaji wa Afya na Mazingira katika jamii.

Afisa Afya na Mazingira Bi Zeldat Masoud Khamis akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe jinsi ya elimu ya afya ya mazingira kwa wanafunzi hao. 
Mafunzo ya vitendo jinsi ya kusafisha mikono kujinginga na maradhi na kuweka mazingira mazuri ya afya yake kwa kutumia maji na sabuni kufanya usafi kabla ya kula na baada ya kutoka msalani.

Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe wakisoma kipeperushi kinachoelezea Afya ya Mazingira wakati wa mafunzo hayo. 
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma vipeperushi vinavyoeleza utunzaji wa Afya na Mazingira ili kujikinga na maradhi ya matumbo na kipindupindu, Mafunzo hayo yanatolewa na Mradi wa Kampuni ya Pennyroyal inayojenga Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar.


Imetayarishwa na Othman Mapara wa Zanzinews.com

Joint UN Women and UNESCO Message for International Women's Day - 08 March 2017

Joint Message from UN Women Representative, Maria Karadenizli and UNESCO Head of Office and Representative for the United Republic of Tanzania, Ms Zulmira Rodrigues on International Women’s Day -Everybody has a stake in promoting equality between men and women, at all levels of society 
“The story of women's struggle for equality belongs to no single feminist nor to any one organization but to the collective efforts of all who care about human rights.” These words by activist Gloria Steinem testify to the universal nature of the fight for women’s rights and once a year, on 8 March, we restate our commitment to gender equality as a force driving dignity for all.
 Inequality between men and women penalizes societies at all levels of development. The violence, injustice and stereotypes suffered by too many women in their personal or professional lives undermine society as a whole, and deprive of it considerable potential for creativity, strength and confidence in the future. 
As the United Nations has adopted the ambitious 2030 Agenda for Sustainable Development, the full empowerment of girls and women is one of humanity’s most powerful levers for development. Rural women are directly responsible for the production of half the world’s food – and it is primarily women who manage and gather natural resources. Ninety per cent of rapes in the world take place precisely when women are on their way to collect water or firewood. 
Two thirds of illiterate adults in the world are women. One in three women is subject to physical violence in the private sphere, and the wage gap between men and women, for equal work and with equal skills, is a fact across the world. For UNESCO, the main engine for change rests on education, training, and the possibility given to all girls and women of pursuing careers in research, politics and culture. Equality also lies in ridding the media and collective imagination of prejudice by highlighting the women scientists, artists and politicians who are moving humanity forward in all fields.
 On the occasion of this 2017 International Women’s Day, UNWOMEN and UNESCO call on all to make a commitment to women’s’ rights, and thereby enhance rights and dignity for all.

ANNA ABDALLAH APONGEZWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI YA TGGA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Tanzania Girl Guids Association (TGGA), Anna Abdallah (kushoto), akipongezwa na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kulia) na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro baada ya kuchaguliwa Dar es Salaam jana. (PICHA ZOTE NA NA RICHARD MWAIKENDAKAMANDA)
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Tanzania Girl Guids Association (TGGA), Anna Abdallah (kushoto),Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kulia) na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro wakipiga makofi wakati wa mkutano huo wa kumtambulisha Anna. 
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Tanzania Girl Guids Association (TGGA), Anna Abdallah (kushoto), akipongezwa na Mjumbe wa Bodi hiyo, Zakia Meghji.
Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba (kulia) akimpongeza Anna Abdallah
Mary akimpongeza Anna Abdallah
Wakiwa na furaha kutoka kushoto ni Grace Makenya, Anna Abdalah, Profesa Martha Qorro na Hangi
Baadhi ya Girl Guids wakiwa katika picha ya pamoja

WANAWAKE WAONGOZA KUWA NA VIRUSI VYA UKIMWI NCHINI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.

Waziri Mhagama alisema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa  kuwa  jumla ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.

“UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa  maambukizo mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo  inaashiria kupoteza  nguvu kazi kubwa katika nchi yetu”

Kwa mujibu wa Waziri Mhagama alisema Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani kuhakikisha wanatokomeza janga la ugonjwa huo  ifikapo mwaka 2030.

Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini  pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.

”Ingawa maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.

UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA KESHO IJUMAA KILIMANJARO.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini walipokutana na wanahabri mkoa Kilimanjaro kuzungumzia tukio la uzinduzi litakalo fanyika kesho Ijumaa katika viwanja vya kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini ,Elizabeth Mushi akizungmza walipkkutana na wanahabari mkoani Kilimanjaro.
Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili kutoka Mtandao wa Jinsia wa jeshi la Polisi (TPF Network) , Grace Lyimo (Kushoto) na Theresia Nyangasa.(Kulia).
Meneja Programu wa Shirika lisililo la Kiserikali linalojishughulisha na kupinga ukeketaji (NAFGEM) Honorata Nasuwa akizungumza mbele ya wanahabri juu ya uzinduzi rasmi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia .
Afisa Programu wa Shirika linalotoa msaada wa Kisheria Kilimanjaro-KIWECO,Hilaly Tesha akizungumza wakati wa mkutano wa na wanahabari kuzungumzia tukio hilo .
Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ,Elina Maro akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano na Wanhabari mkoa wa Kilimanjaro ukiendelea.
Baadhi ya Wanahabri mkoa wa Kilimajaro wakiwa katika mkutano huo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAWAKILISHI WA WANAWAKE WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO NA KUWEKA MAAZIMIO YAO WAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kijana wa Kitanzania aliyekuwa kwenye msafara wa Kilimanjaro, Judith Severin (wa pili kutoka kulia) akisoma tamko kuhusu yaliyojadiliwa katika kongamano la wanawake ambao ni wakulima wadogo wadogo waliokuwa kujadili changamoto na kutoka na maadhimio hasa katika suala la kumiliki Ardhi.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bi Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyowasimamia wanawake wa Tanzania waliowawakilisha wenzao katika kongamano la wanawake lililiofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Mwanamke aliyefika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, Flola Matiasi  akizungumza na vyombo vya habari kuhusu alivyofanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kusimika maadhimio hasa umiliki wa ardhi kwa wanawake.
Maneja wa Programu ya Ushawishi na Utetezi, Grace Kisetu akitoa ufafanuzi wa swali lililoulizwa na mwandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa TGNP Mtandao.
Meneja Kilimo na Haki ya Ardhi kutoka Action Aids , Elias Mtinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango Action Aids katika kupigania haki za wanawake hapa nchini Tanzania.
Baadhi ya wanawake waliowawakilisha wenzao katika Kongamano lililofanyika Mkoani Kilimanjaro na kuwakutanisha wanawake kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

YALIYOJIRI KATIKA KONGAMANO LA WAWAKILISHI WA WANAWAKE KUTOKA AFRIKA WALIOKUTANA KUJADILI MADAI YAO YA UMILIKI WA ARDHI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wawakilishi wa Wanawake kutoka nchini Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja  wakati wa kuwapokea wanawake waliopanda mlima Kilimanjaro na kusimika madai yao juu ya umiliki wa Ardhi.
Wawakilishi wa wanawake wa Uganda  wakiwasubilia wanawake wenzao waliopanda mlima Kilimanjaro.

Wawakilishi wa wanawake kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiimba nyimbo mbalimbali walipokuwa wanaelekea eneo la Marangu lilipo geiti la kupandia mlima Kilimanjaro ili kuwapongeza wanawake waliopanda mlima kilimanjaro na kufika katika kilele cha mlima huo na kuweka madai yao hapo.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Tanzania wakiwapokea wanawake wawili waliofanikiwa kufika kilele cha mlima Kilimanjaro na kuweka Madai ya hasa la mwanamke kupata haki sawa katika kumiliki Ardhi
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akimpongeza Tatu Maleta(aliyekaa) aliyefanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuweza kuweka madai ya kupata haki ya kumiliki ardhi.Aliyekaa upande wa kulia ni  Bi. Flora Matiasi aliyefanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro.
Wanawake wa Kitanzania waliofanikiwa kufika kilele cha mlima Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wanawake wa Tanzania
Wanawake wa Kitanzania wakiwa wanajiandaa kuingia ukumbini kwa ajili ya kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika waliokutana katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Nigeria wakiingia ukumbini wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Malawi wakiingia ukumbini wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Uganda wakicheza kwa firaha wakati wa kuingia ukumbini wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwaongoza wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Tanzania wakati walipokuwa wakiingia ukumbini kwa ajili ya ufungajiwa kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Tanzania wakiserebuka kwa furaha
Baadhi ya wanawake kutoka barani Afrika waliokutana katika ukumbi wa Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha

Mwanamziki na Mwanaharakati wa Haki za wanawake, Sister D kutoka nchini Zambia akitoa burudani wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake kutoka nchini mbalimbali barani Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Mwanamziki na Mwanaharakati wa Haki za wanawake, Michael kutoka nchini Zambia akitumbuiza wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake kutoka nchini mbalimbali baran Afrika.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Dkt. Vincensia Shale akizungumza jambo wakati wa kufunga kongamano hilo
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi(kushoto)akifuatilia kongamano
Maneja wa Programu ya Ushawishi na Utetezi, Grace Kisetu(aliyeshika kipaza sauti) akisoma  wasifu wa viongozi waliopewa tuzo za mchango wao katika kupigania haki ya wanawake.
Mratibu wa Kituo cha usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akipokea tuzo kwa niaba ya Thabisa Siwale ambaye ilipigania haki ya wanawake kupata ardhi kwenye ukumbi wa  Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Mke wa Marehemu Saidi Augustino akipokea tuzo ya mume wake aliyekuwa jaji na kuwapiania wnawake kupata haki zao katika jamii kwenye ukumbi wa  Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.