JACK WOLPER: ''NIMECHOKA KUTAPELIWA KIMAPENZI NA SIHITAJI KULIA TENA"
By: VIJIMAMBO on October 31, 2012 / comment : 0
Wapambe hao ambao mara nyingi huwa karibu na msanii huyo, walifunguka kuwa kwa sasa msanii huyo hana mwanaume na endapo akimpata basi ataamua kufanya hivyo ili kuzuia matatizo mengine yanayoweza kutokea kama kuibiwa na watoto wenyewe njaa kali wanajifanya wamesomea mapenzi.
Hata hivyo walidai kuwa kingine ambacho msanii huyo hataki kukosea tena ni kumtangaza mpenzi wake kwa mademu wa bongo movie kwani wanahusika mara kadhaa kwa kuharibu mapenzi yake kwani hawakawii kufanya mapinduzi.
“Ishu iko hivyo mjini hapa kila mtu ana mipango lakini kwa upande wa mwanadada Wolper mambo yako hivyo na hataki kupoteza muda kwa sababu mademu wa tasnia hiyo wana tabia ya kumzoea mtu kwa dakika kadhaa baada ya hapo kwisha habari wanaondoka mwanaume kama hawana akili nzuri,” alisema mpambe.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta Wolper ili kutoa la moyoni naye alidai kuwa lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja hivyo anachopanga sasa anaamini kitatimia kwani amechoka na wezi wa mapenzi ambao mwisho wa siku wanaachana kwa vita na maneno ya kudhalauliana.
Rushwa nje nje uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM
By: VIJIMAMBO on October 31, 2012 / comment : 0
WAPAMBE NUSURA WAZICHAPE KAVUKAVU, UCHAGUZI KUFANYIKA DODOMA LEO
Uchaguzi huo wa wazazi ndiyo wa funga dimba la mfululizo wa chaguzi za chama hicho tawala kuanzia ngazi za shina tangu Aprili.
Tuhuma hizo za rushwa zimejitokeza licha ya juzi wagombea mbalimbali kukaririwa wakiyakana makundi ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa na ajenda maalumu ya kusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia chama hicho.
Mmoja wa wajumbe kutoka mkoani Iringa alimwambia mwandishi wetu kuwa tayari baadhi ya wajumbe wanaoonekana kuwa na msimamo mkali wamekuwa wakipewa Sh100,000 kila mmoja wakati wajumbe wengine wamekuwa wakihongwa kati ya Sh40,000 na 70,000.
“Nikimwona Rais Jakaya Kikwete nitamwambia. Hali hii siyo nzuri na haiwezi kuvumiliwa. Kama alivyosema juzijuzi hapa nilimsikia, lazima achukue hatua, la sivyo chama chetu kitakufa,” alisema mjumbe huyo ambaye aliomba asitajwe jina.
Katika hatua nyingine, makundi ya baadhi ya wajumbe waliokuwa wameketi katika moja ya baa maarufu mjini Dodoma, juzi usiku walitimka mbio baada ya kuona gari likiegeshwa pembezoni mwa baa hiyo.
Wajumbe hao waliokuwa kwenye harakati za kupanga mikakati ya kuzunguka katika nyumba za kulala wageni kwa ajili ya ‘kuonana’ na wajumbe, walitimka wakidhani kuwa gari hilo lilikuwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Wagombea wanaowania uenyekiti, John Barongo na Abdallah Bulembo juzi, kwa nyakati tofauti walikanusha kuwa na maslahi na makundi yanayodaiwa kushiriki katika vitendo vya kutoa rushwa katika uchaguzi huo unaofanyika leo. Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Martha Mlata alikataa kuzungumzia uchaguzi huo.
Uchaguzi huo, unahitimisha uchaguzi wa jumuiya tatu za chama hicho, baada ya ule wa UWT na UVCCM ambazo zilizua malalamiko kutokana na kutawaliwa na madai ya rushwa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifunga mkutano wa UWT na baadaye alipofungua ule wa UVCCM, alikemea vitendo hivyo na kueleza athari za rushwa katika chaguzi za chama.
Mchuano wa Wabunge
Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa UWT, mchuano mwingine mkali unaonekana katika kinyang’anyiro cha ujumbe wa Nec, huku kukiwa na idadi kubwa ya wabunge wanaowania nafasi hiyo.
Majina 16 yamepitishwa kuwania viti vitatu vya Nec kwa upande wa Tanzania Bara, wakati kwa upande wa Tanzania Visiwani majina yaliyopitishwa ni saba kugombea nafasi mbili.
Miongoni mwa wanaowania nafasi tatu Bara ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, Stella Manyanya na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu.
Pia wamo wabunge ambao majimbo yao yapo kwenye mabano Said Bwanamdogo (Chalinze), Vita Kawawa (Namtumbo), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) na Mbunge wa zamani wa Viti Maalumu, Esther Nyawazwa.
Wengine katika kundi hilo ni Norad Kigola, Priscilla Mbwaga, Dk Salim Chikago, Jeremia Wambura, Bernard Murunya, Thobias Mwilapwa, Paulo Kirigini na Clementina Mollel.
Kutoka Zanzibar, wanaowania nafasi mbili za Nec ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Perera Ame Silima, Abdulla Khamis Feruz, Ali Suleiman Othman, Fatuma Abeid Haji, Panya Ali Abdalla, Twaha Ally Muhajir na Hassan Rajab Khatib.
Pia mkutano wa leo unatarajiwa kumchagua Makamu Mwenyekiti, nafasi inayowaniwa na Hassan Rajab Khatib, Ali Issa Ali na Dogo Iddi Mabrouk.
Utawachagua pia wajumbe wa Baraza Kuu la Wazazi na wawakilishi wa jumuiya hiyo katika mabaraza ya UVCCM na UWT.
Vijembe vya Kampeni
Kampeni zimekuwa zikipamba moto kadri muda wa uchaguzi unavyokaribia na mbinu mbalimbali zimekuwa zikitumika ili kujihakikishia ushindi.
Magari mengi yamepambwa picha nyingi za wagombea, wapambe wanapita sehemu mbalimbali kuomba kura na kuta za uzio wa ofisi za CCM zimechafuka kwa picha za wagombea.
Ushindani mkubwa unaonekana kuwa baina ya Barongo na Bulembo ambao jana walikuwa kivutio kikubwa walipokutana katika ofisi za CCM Makao Makuu, Dodoma ambako walikumbatiana kisha kuanza kurushiana vijembe.
Bulembo alisema: “Nilipomkuta anachukua fomu, nilimwuliza mwalimu wangu huyu (Barongo) kwamba nilidhani kwamba sasa unaniachia nikutue mzigo, kumbe bado tena nawewe unagombea?”
Barongo alimjibu akisema: “Hilo haliwezekani kabisa, ujue ninyi bado watoto hamjakomaa bado mnahitaji kuongozwa, kwa hiyo wewe tulia kwanza muda mwafaka ukifika nitakukabidhi.”
Jana asubuhi, Bulembo alifika katika Viwanja vya Bunge kuomba kura kwa baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo.
Muda mfupi kabla ya wabunge kuingia ukumbini, Bulembo alikuwa nje ya lango kuu la kuingilia kwenye ukumbi wa Bunge na kila mbunge aliyejitokeza alimsalimia kisha kuomba kura kwa wale ambao ni wajumbe hao.
Mlata jana kwa muda mrefu hakuonekana katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM na taarifa zinasema huenda alikuwa akihudhuria kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo kilichofanyika jana katika Chuo cha Mipango.
Licha ya kutokuwapo kwake, kulikuwa na vijana wachache waliokuwa wamevalia mabango makubwa yenye picha yake, vifuani na kwenye migongo yao wakimpigia kampeni.
Wafuasi nusura wazichape
Wakati Bulembo na Barongo wakirushiana vijembe kwa furaha, watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wao nusura wachapane makonde walipokuwa wakiimba nyimbo za hamasa CCM Makao Makuu.
Wafuasi hao jana walikuwa wakizunguka wakiwa na mabango yenye kuwanadi wagombea hao katika ofisi hizo kati ya saa sita na saa nane mchana huku wakiimba nyimbo za hamasa.
Hali hiyo ilisababisha kutosikilizana katika eneo hilo, hivyo kuwalazimu maofisa wa CCM kuviamuru kuondoka na kuelekea katika mbele ya jengo la vikao vya NEC maarufu kama White House. Viliitikia wito na kwenda huko ambako viliendelea kuimba nyimbo za hamasa.
Wakati vikiwa katika eneo hilo, wafuasi hao walianza kurushiana maneno makali kwa huku kila upande ukidai kufanyiwa rafu na upande mwingine, hali iliyozua tafrani iliyodumu kwa zaidi ya dakika 20.
Hata hivyo baadhi ya makada wa pande hizo mbili, walitumia busara na kuwatuliza na kila kikundi kuelekea upande tofauti na kuhitimisha shamrashara hizo.
RATIBA YA MKUTANO WA TISA WA BUNGE TAREHE 30/10/2012 MPAKA 09/11/2012
By: VIJIMAMBO on October 30, 2012 / comment : 0
TAARIFA KWA UMMA
By: VIJIMAMBO on October 30, 2012 / comment : 0
Mchungaji Lwakatare Atoa Ujumbe Wa Amani
By: VIJIMAMBO on October 30, 2012 / comment : 0
Kova kuanza kusaka mtandao wa vipeperushi
By: VIJIMAMBO on October 30, 2012 / comment : 0
Hatua hiyo imekuja baada ya waumini hao kupanga kufanya maandamano Novemba Mosi, ambayo yatahamasisha mahakama hiyo kutoa dhamana kwa kiongozi wa taasisi hiyo na wenzake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema wataanza kufanya msako wa wote wanaohamasisha, wanaochapisha na wanaotoa vipeperushi ili kuwakamata.
“Tunafuatilia wadhamini na wachapishaji wa vipeperushi kwani ni chanzo cha uchochezi na upotevu wa amani nchini,” alisema Kova.
Kova alisema maandamano hayo ambayo yamepangwa na waumini hao yanatishia amani , wananchi watashindwa kwenda kazini na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
“Hatuna mazungumzo tena kwa suala lolote litakalotishia uvunjifu wa amani hasa kwa yeyote atakayefanya maandamano bila kibali, hatutangalia anatoka dini gani au chama gani hivyo polisi itafanya kazi yake na kuwachukulia hatua kali,” alisema Kova na kuongeza:
“Kisheria kumtishia mtu siyo lazima utumie bomu, bali unaweza ukatumia kauli au vipeperushi kama hivyo vya maandamano.”
Alisema wazazi watakaoruhusu watoto wa shule kufanya maandamano watachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani, ikiwezekana kufungwa mwaka mmoja jela.
“Nimesikia wanataka kuwahusisha watoto wasiende shule, ili wafanye maandamano ambayo yanazuiwa na sheria ya mtoto kutofanya maandamano,” alisema Kova na kuongeza:
“Sisi tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake, kama kuna mtu amefikishwa mahakamani kuna taratibu zake za kupata dhamana, siyo kufanya maandamano haramu.”
Pia, aliwaomba wananchi wasishiriki maandamano hayo kwani yataleta madhara makubwa kwa familia zao kwa wale watakaokamatwa.
“Hii inajidhihirisha pale utakapotembelea familia za wale waliokamatwa katika maandamano yaliyopita, watoto wanashindwa hata kwenda shule kutokana na kukamatwa kwa wazazi wao na wanakosa nauli na chakula,” alisema Kamanda Kova.
Pamela Chilongola, Nuzulack Dausen na Zaina Malongo
INJINIA MANYANYA AJITOSA KUTETEA NAFASI YAKE YA UJUMBE WA NEC TAIFA KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI
By: VIJIMAMBO on October 30, 2012 / comment : 0
Kuna Uhaba Mkubwa Wa Mafuta Nchini Kwa Sasa
By: VIJIMAMBO on October 30, 2012 / comment : 0
Hapana! Bahati nzuri dereva wa basi la kwenda Uhambingeto aliweza kunisaidia kwa kuniuzia lita zake ishirini za dizeli. Zinifikisha Mikumi. Pale Mikumi nikafanikiwa kupata mafuta ya kununua kituoni. Vinginevyo, kwa mara ya kwanza jana nimelazimika kununua mafuta ya ' kulanguliwa'. Lita moja kwa shilingi elfu tatu. Hakyamungu!
Songea
Mjini Singida
Wingu laigubika Ripoti ya Ngwilizi
By: VIJIMAMBO on October 30, 2012 / comment : 0
WAKATI Bunge likianza mkutano wake wa Tisa leo, zipo taarifa Ripoti ya Kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa haitasomwa na kisha kujadiliwa.
Badala yake, kwa mujibu wa watoa habari wetu, Kamati ya Uongozi, iliyokutana jana iliamua kwamba litatolewa tamko kuhusu ripoti ya kamati hiyo, hivyo haitasomwa wala kujadiliwa kama ambavyo wabunge wamekuwa wakitaka.
Kwa maana hiyo Spika wa Bunge, Anne Makinda huenda akatumia kanuni nyingine kutoa tamko kuhusu uchunguzi huo, hali ambayo haitatoa fursa kwa wabunge kuijadili kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakishinikiza.
Miongoni mwa kanuni ambazo Spika anaweza kuzitumia ni pamoja na ile ya 33 (2) ambayo inasema: “Wakati wa kikao, Spika anaweza kutoa taarifa nyinginezo kadri atakavyoona inafaa.”
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel jana alikataa kuzungumzia suala hilo akiahidi kulitoa ufafanuzi leo... “Ratiba ya shughuli za Bunge bado iko kwenye ngazi ya Kamati ya Uongozi. Sasa pengine tusubiri kesho (leo) ikiwa tayari kila kitu kitakuwa wazi, hakuna haja ya kuwa na haraka.”
Jana, Kamati ya Uongozi wa Bunge ilikutana mjini Dodoma kujadili mambo mbalimbali na habari zinasema kwamba suala la Ripoti hiyo ya Ngwilizi, pia lilijadiliwa.
Agosti 2 mwaka huu, Spika Makinda aliunda kamati hiyo ndogo kuchunguza tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya wabunge ambao walidaiwa kwamba walihongwa ili kuikwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kuundwa kwa kamati hiyo, kulitanguliwa na tukio la kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Julai 28, mwaka huu pia kutokana na tuhuma hizohizo.
Tayari kumekuwa na taarifa kwamba ripoti hiyo imevuja na maudhui yake kuchapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari, hali ambayo ilisababisha Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuonya kwamba waliohusika na kuvuja huko huenda wakajikuta matatani kwani ni kosa la kisheria.
“Kitendo cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo katika vyombo vya habari ni kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 31 (1) (g) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura 296,” alisema Ndugai katika mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni.
Mmoja wa wabunge ndani ya kamati iliyochunguza suala hilo (jina tunalihifadhi kwa sasa), ndiye anayedaiwa kwamba aliivujisha ripoti hiyo ya uchunguzi kwa makusudi, lengo likiwa ni kumshinikiza Spika Makinda aitoe hadharani ili kuwasafisha watuhumiwa.
Mbunge huyo alifanya hivyo kwa msukumo wa baadhi ya wabunge waliotuhumiwa kujihusisha na rushwa, pamoja na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kabla ya kuvunjwa.
Kadhalika, Ndugai katika mkutano wake na vyombo vya habari alisema suala la ripoti hiyo kusomwa bungeni au vinginevyo linategemea uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge.
Ndugai alisema baada ya kamati kuwasilisha ripoti kwa Spika, Kamati ya Uongozi ya Bunge itakaa kujadili na kama itaona kuna umuhimu wa kuingizwa katika ratiba ya vikao vya Bunge ijadiliwe.
Alisema Vifungu 114 (17) na 119 (1) hadi (6) vya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007 kwa pamoja vinampa madaraka Spika kuhusu utaratibu wa kufuata katika uwasilishaji wa taarifa bungeni.
Kamati hiyo iliyoundwa na Spika ilikuwa chini ya Ngwilizi ambaye ni Mbunge wa Mlalo, ina wajumbe; Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki), Goesbert Blandes (Karagwe) na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Omary Juma. Kamati hiyo ilimaliza kazi yake na kuiwasilisha kwa spika tangu Septemba 20 mwaka huu.
Kamati za Vyama
Kamati za vyama bungeni zinatarajiwa kufanya vikao vyake leo asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja alisema
Kamati nyingine za Bunge hazijakutana kutokana na wabunge wengi kuwa safarini kwenda mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge.
“Kwa taarifa tulizopokea sasa ni kwamba kamati zimeshindwa kukutana kutokana na wabunge wengi kuwa njiani kuja mjini hapa, hivyo kwa vyovyote kesho (leo) Bunge litakuwa ni fupi ili wabunge wapate nafasi ya kuandaa utaratibu mzima wa ratiba za vikao,” alisema Minja.
Alisema leo mara baada ya kuanza kwa kikao hicho, Bunge litatoa nafasi ya maswali na majibu ambayo Serikali itayajibu kabla ya kuahirishwa.
Mara baada ya kuahirishwa saa nne asubuhi, kamati za vyama zitakutana kupitia mambo mbalimbali kabla ya kuingizwa kwenye kamati mbalimbali za bunge.
Moja ya mambo yanayotarajiwa kutawala katika kamati za vyama ni pamoja na wabunge wa CCM kujiweka sawa kwa ajili ya kusaidia kupitishwa kwa ripoti ya Kamati ya Ngwilizi.
Kingine kitakachojadiliwa katika Mkutano huu wa Bunge ni muswada binafsi kuhusu fao la kujitoa la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tayari Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jaffo na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika wamewasilisha miswada yao kwa Katibu wa Bunge, Tomas Kashillilah.
CHANZO: MWANANCHI
Mjomba Kumbuka Japo Wanao.....
By: VIJIMAMBO on October 29, 2012 / comment : 0
Mfanyakazi wa Barrick mwaathirika wa kemikali afariki
By: VIJIMAMBO on October 29, 2012 / comment : 0
Alipoulizwa kuhusu kifo hicho, Ofisa Habari wa Barrick, Nector Foya alisema hana taarifa za kifo cha mfanyakazi huyo.
Dodoma kuwaka moto, Bunge kuanza Mkutano wa Tisa Kesho
By: VIJIMAMBO on October 29, 2012 / comment : 0
Vigogo 10 wahusishwa mabilioni ya Uswisi
By: VIJIMAMBO on October 29, 2012 / comment : 0
Vigogo wametajwa kuhusika katika kashfa ya kuficha Sh303.7 bilioni katika benki mbalimbali nchini Uswisi.
Katika orodha hiyo inadaiwa kuwa yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).
Majina hayo ambayo mwandishi wetu amefanikiwa kuyaona, yamo katika orodha ya mchunguzi mmoja wa kimataifa wa masuala ya ufisadi (jina tunalo).
Juzi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alimshukia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akimtuhumu kuandika barua Uswisi akisema Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki zilizopo nchini humo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha madai hayo akisema hajawahi kufanya hivyo.
Akizungumza jana Zitto alisisitiza kauli yake akisema: “Sijawahi kumsema Dk Hoseah kwa lolote, kwa nini leo nimsingizie? Yeye mwenyewe anajua ushirikiano niliompa wakati wabunge wanapinga yeye asichunguze malipo ya posho mara mbili kwa wabunge.”
“Nilisimama kidete kusema Takukuru wapo sahihi na mimi nilikwenda mwenyewe kwao kuhojiwa na kuagiza wajumbe wa kamati yangu (Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma), waende kuhojiwa. Spika aliyestaafu (Samuel Sitta) akaizima kashfa ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili. Mwulizeni amesahau? Sasa leo nimzushie ili iwe nini?.”
Alisema orodha ya Watanzania wenye fedha huko Uswisi, ipo na ameiona na nyaraka zinaweza kutolewa kwa taasisi za Serikali tu.
“Dk Hoseah kazuia nyaraka hizo. Akitaka nimwonyeshe mtu anayeweza kutoa nyaraka hizo, nipo tayari isipokuwa aahidi kuiweka wazi,” alisema Zitto.
Alisema katika orodha ambayo Waziri wa Fedha wa Ufaransa anayo, kuna Watanzania lakini akaituhumu Serikali akisema haitaki kufuata njia halali za kupata orodha hiyo kwa kuwa viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa wana akaunti katika benki za Uswisi.
Juni 26, mwaka huu gazeti hili lilichapisha habari kuhusu utoroshwaji wa fedha hizo na kueleza kuwa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na Takukuru inachunguza suala hilo.
Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kuingizwa katika akaunti za Watanzania na kampuni moja ya uchimbaji mafuta na kampuni kadhaa za uchimbaji madini ambazo zinafanya kazi Tanzania.
Chanzo hicho kiliongeza kwamba kiasi hicho cha fedha kipo katika akaunti sita tofauti zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa wakubwa.
Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi.
“Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti ambazo zinamilikiwa na wanasiasa wakubwa nchini na wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini,” kilidokeza chanzo hicho.
Kugundulika kwa kiasi hicho cha fedha katika benki za Uswisi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB) iliyotolewa mwaka huu.
CHANZO: MWANANCHI
Magazet Leo Jumatatu Tarehe 29/10/2012
By: VIJIMAMBO on October 29, 2012 / comment : 0
Kichanga afariki dunia baada ya kukeketwa
By: VIJIMAMBO on October 29, 2012 / comment : 0
WATU wawili mkoani Singida wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwamo la mtoto mwenye umri wa miezi minne kupoteza maisha baada ya kukeketwa.
CHANZO: MWANANCHI
MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa Mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, Ametangaza Kujivua Uanachama
By: VIJIMAMBO on October 28, 2012 / comment : 0
|
-Awaasa vijana kuwa mabadiliko ndani ya Tanzania si kuiondoa CCM
na kuiweka Chadema.
|
| Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa mbeya na iringa wakimsikiliza mlezi Thomasi Nyimbo katika ukumbi wa hotel yake ya Maunt livingstone jijini mbeya |
| Raymond wa Ebony FM Iringa na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu wakiwa makini kumsikiliza mzee Nyimbo |
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
* Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) Unatoa Ufafanuzi Kuhusu Mkutano wa Ikulu Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) unapenda kutoa ufafanuzi...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, today held talks with the Acting United States Ambass...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, M...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015












