Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal akizungumza kwa niaba ya
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete katika Hafla ya Usiku
wa Mwanamke Mjasiriamali ya kuchangisha fedha kwa Wanawake
Wajasiriamali ikiwa ni Kipindi cha Mwezi wa Wanawake Wajasiriamali
nchini wenye Kauli mbiu "Msichana Amka Ujasiriamali ni Ajira" ambapo
amewataka Wakinamama waliokwisha fanikiwa kuwaongoza Wasichana na
wajasiriamali wanaochipukia njia sahihi za kibiashara zitakazowawezesha
kufikia mafanikio katika biashara na kutumia ubunifu wao kama
rasilimali.
Mjasiriamali
na Mkufunzi Bi.Namsifu Nyagabona akishirikishana uzoefu wa Biashara na
wanawake wajasiriamali katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali
iliyohudhuriwa na Wabunge Wanawake pamoja na Wake za Viongozi
uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es
Salaam
Meza kuu ikisikiliza Shuhuda za
Kinamama waliofanikiwa katika Biashara za Ujasiriamali. Mgeni rasmi
katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasirimali Mama Asha Bilal (wa tatu
kulia), Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda( wa pili kulia), Mwenyekiti
wa Bodi ya WAMA Bi. Hulda Kibacha (kulia), Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi.
Hopolang Phororo (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira), Dk. Therezya Huvisa (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa
Taasisi ya MOWE Bi. Elihaika Mrema (wa tatu
kushoto)\
Baadhi ya
Wake za Viongozi, Wabunge Wanawake na Wanawake Wajasiriamalia
waliohudhuria hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali iliyofanyika
jijini Dar es Salaam Serena
Hotel.
No comments:
Post a Comment