HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Dar: Wagonjwa wa Ilala wadaiwa kukimbilia Kisarawe

HOSPITALI ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani imeelemewa na wagonjwa kutokana na wimbi la wakazi wa Dar es Salaam kukimbilia kupata huduma hospitalini hapo.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Paschal  Dk Nkii alisema uwingi wa wagonjwa hao umesababisha kuwapo kwa upungufu wa vifaa upande wa kutolea huduma ya meno.

 Dk Nkii alisema hayo baada ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kuadhimisha Siku ya Mlipa Kodi nchini.

Alisema wagonjwa wengi wanaowahudumia katika hospitali hiyo, wanatoka maeneo ya Gongolamboto, Chanika, Pugu na Ukonga wilayani Ilala, ambayo kijografia yapo jirani na wilaya hiyo.

 ” Upande wa huduma ya meno hatuna vifaa kabisa, lakini wagonjwa wengi tunaowahudumia wanatokea jijini Dar es Salaam, hivyo tunaiomba Serikali na wadau wa taasisi mbalimbali wajitokeze kusaidia kununua vifaa vya meno”alisema Dk Nkii. Alisema dawa zinazohifadhiwa katika hospitali hiyo zinaharibika kutokana na mashine ya kiyoyozi iliyopo katika chumba cha kuhifadhia dawa hizo kuwa mbovu. “Kwa upande wa dawa tunahitaji mashine ya kiyoyozi ili kuzuia dawa zisiharibike, kwani iliyopo imeharibika”alisema Dk Nkii. Alishukuru kupata msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambavyo thamani yake ni Sh13.5 milioni.

 Alisema vifaa walivyopokea ni mashine ya kutoa uchafu kwa njia ya hewa kwa mtoto aliyezaliwa, vitanda sita, magodoro sita na mashine tano kwa ajili ya kupima ugonjwa wa shinikizo la damu ambapo vifaa hivyo vitatumiwa katika wodi ya wazazi.
Akizungumza machache baada ya kukabidhi, Naibu Kamishna wa TRA ,Rished Bade alisema wamejumuika na jamii katika siku ya maadhimisho ya mlipakodi kwa kutoa msaada wa vifaa katika wodi ya wazazi. “Tumetumia nafasi hii ya maadhimisho haya kusaidia hospitali hii vifaa vya wodi ya wazazi ambavyo tumenunua kutokana na kodi za wananchi,”alisema Bade.

CHANZO: MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: