LIGI
Kuu ya Tanzania bara mzunguko wa pili ipo kwenye hati hati ya
kutofanyika baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuzifungia
akanti za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na TFF kudaiwa
zaidi ya milioni 100 na TRA.
Hatua
hiyo ya TRA ya kuzifungia akaunti hizo za TFF, imekuja baada ya TFF
kukiuka taratibu za kuwakatia kodi makocha wa kigeni wanaozifundisha
timu za Taifa tangu kipindi cha Mbrazil Marcio Maximo.
Akizungumza
kwenye ukumbi wa hostel za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kaimu
katibu mkuu wa shirikisho hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi,
Sunday Kayuni alisema kutokana na hatua ya TRA kuzifungia akaunti hizo
huenda Ligi Kuu mzunguko wa pili isifanyike kutokana moja ya akaunti
hizo kuwa na zaidi ya Sh.350m za klabu ambazo zimetoka katika kampuni
ya Vodacom ambayo ndiyo mdhamini wa ligi hiyo.
"Akaunti
zetu zote zimesimamishwa na TRA kwa kile kilichodaiwa kuwa hatujalipa
zaidi ya sh 100 milioni za kodi za mishahara ya makocha wote waliowahi
kuzifundisha timu za taifa kuanzia kipindi cha Maximo hadi
Sasa."alisema Kayuni ".
Kufatia
hali hiyo kunauwezekano mkubwa wa Ligi Kuu mzunguko wa pili kutofanyika
kwa sababu moja ya akaunti hizo ilikuwa na zaidi ya sh 350 za klabu
kutoka Kampuni ya Vodacam wadhamini wakuu "Wote tunafahamu kuwa hali
halisi ya klabu zetu kiuchumi hivyo kufungiwa kwa akaunti hizo
kutaathiri moja kwa moja mchakato mzima wa ligi kwani timu nyingi
zinategemea fedha hizo kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na maandalizi ya
ligi" alisema Alisema.
TRA
kufungia akaunti za TFF, imekiuka taratibu za kodi kwani shrikisho hilo
halipaswi kulipa kodi hiyo kwa sababu siyo linalolipa mishahara ya
makocha hao. Alisema Kodi hiyo ilipaswa kulipwa na Serikari ambayo ndiyo
inayolipa mishahra ya makocha hao na siyo TFF.
"Hakika hatujatendewa haki na huu ni uonevu, hatahivyo pia tumejaribu kufuatilia lakini tumekuwa tukipigwa danadana....."
Pia
tunasikitika Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo
haionyeshi ushirikiano juu ya jambo hili ambalo linatufanya tuone kuwa
kuna kitu hapo katikati," alisema Kayuni ambaye alikuwa samabamba na
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Said Mohamed pamoja na Mtendaji Silas
Mwakibinga.
Katika
hatua nyingi Kayuni alisema kuwa wapo kwenye mchakao wa kuunda kamati
maalum itakayohusisha TFF pamoja na wawakilishi wa klabu ili iweze
kukutana na TRA kwa mara nyingine tena kuangalia uwezekano wa kutatua
tatizo hilo.
Hata
hivyo Kayuni alisisitiza kuwa TFF haitalipa kodi hizo na haina fedha za
kulipa sababu siyo inayotakiwa kufanya hivyo kwa mijibu wa sheria ya
kodi sababu siyo inayolipa mishahara ya makocha hao.
No comments:
Post a Comment