HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Rais Jakaya Kikwete awasha moto Jumuiya ya Wazazi

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema kwa mara nyingine, CCM lazima itafute dawa ya kuondokana na rushwa wakati wa uchaguzi.

Mbali na hilo, Rais Kikwete amewataka viongozi wapya wa Jumuiya ya Wazazi kuthibitisha kwa vitendo kwa nini jumuiya hiyo, isifutwe kutokana na kushindwa kutimiza malengo ya kuundwa kwake.


Akifunga mkutano wa Jumuiya ya Wazazi jana, Rais Kikwete alisema wagombea wamekuwa na tabia ya mbaya kununua uongozi, hali inayokitia aibu chama hicho.

”Tabia ya kununua ushindi kwa kuwapa fedha wajumbe ili wakuchague ni mbaya, hili nimelisema katika jumuiya zote na ninarudia kulisema, ni aibu ambayo lazima tuitafutie dawa ya kuondokana nayo.

”Kwa wale wanaonunua uongozi na wale wanaofurahishwa kwa kupewa Sh 30,000 ambayo imenufaisha yeye binafsi ajue kuwa sura ya chama imeathirika sana, utafurahia kupata fedha hizo, lakini athari ya chama kwa jamii ni kubwa.

”Chama chetu, kinaonekana ni cha watoa rushwa, watu wa kununua kura, kwa kweli hili siwezi kuacha kulisema, mliyoyafanya mnayajua na wengine mpo humu ndani,” alisema Rais Kikwete.

Akizungumzia kuhusu jumuiya hiyo, alisema karibu atashindwa kuibeba jumuiya hiyo kutokana na malalamiko mbalimbali, hasa katika vikao vya Halmashauri Kuu (NEC) ambapo hoja nyingi za kutaka kufutwa kwa Jumuiya ya Wazazi huibuka.

Alisema hali hiyo, inatokana na ubadhirifu wa fedha na mali za jumuiya, hali inayosababisha ishindwe kujiendesha.

Alisema Jumiya ya Wazazi, imeshindwa kuisaidia CCM kupata ushindi katika chaguzi mbalimbali tofauti na jumuiya nyingine kama Jumuiya ya Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

”Shule zenu zimekuwa ndio mzizi wa fitina, kusikia taarifa za ubadhirifu wa fedha za shule imekuwa ni jambo la kawaida, shule zenu nyingi hazifanyi vizuri na hazitoi elimu bora,” alisema.

Alitoa mfano wa shule ya Kaole iliyopo Bagamoyo, ambayo Jumuiya hiyo ilirithishwa na Chama cha FLELIMO cha Msumbiji ambayo tayari majengo yake yamebomolewa na viongozi waroho wa fedha, hali inayosababisha historia kupotea.

“Ninyi viongozi wapya kaeni chini mjiulize kulikoni? Rejesheni heshima ya Jumuiya ya Wazazi na mthibitishe kwa vitendo kwa nini jumuiya hii isifutwe, maana hoja za kuifuta ni nyingi kuliko hoja ya kuiacha iendelee,” alisema.

Alisema hataki jumuiya hiyo isiwe mzigo kwa chama, badala yake ifufue vyanzo vyake vya mapato kama vile shule, viwanja na majengo pamoja na kuvisimamia vizuri ili iweze kujiendesha yenyewe.

Rais pia amesisitiza viongozi wapya kuvunja makundi yaliyokuwepo ili wawe kitu kimoja kwa ajili ya kuimarisha jumuiya.

"Jumuiya sio mali ya walioshinda na kambi yao, kila mtu apewe fursa sawa ya kuitumikia jumuiya, kiongozi atakayeendeleza makundi na visasi hana sifa ya kuendelea kuwa kiongozi.


CHANZO: MTANZANIA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: