STAA wa sinema za Bongo, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ amewafungukia mastaa wawili maarufu wanaoeneza habari kwamba yeye ana ‘ngoma’, Amani linakudondoshea.
Akizungumza na waandishi wetu juzikati, Steve alisema mastaa wanaosambaza habari hizo ni watu wake wa karibu kwa muda mrefu huku wakishirikiana kwa kila jambo.
Alisema maneno hayo yaliongewa na mastaa hao kwenye hoteli moja maarufu, jijini Dar na baadaye kumfikia mke wake kitendo kilichomfanya mke huyo kulia.
“Afadhali maneno hayo ningeyasikia mimi tu, lakini hadi kwa mke wangu yamefika na kumuathiri sana,” alisema Steve.
Pamoja na maneno hayo, mchekeshaji huyo alisema kuwa amewasamehe wote walioshiriki kuyazua na wala hana kinyongo na yeyote.
“Nadhani wamejisahau kuongea bila kuwa na ushahidi na Mungu atawalipia, ninachotaka kusema sina kinyongo na mtu,” alisema Steve.
Baada ya kupata tuhuma hizo, Amani lilimtafuta Mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Huo ni uzushi namba moja, kwanza ningependa kujua unaihusu Bongo Movie? Na kama Steve anawajua hao wanaomzushia basi alete ushahidi mara moja maana tupo kwa ajili ya kutengeneza umoja na si malumbano.”
Kwa upande wake, Katibu wa Bongo Movie, Salum Mchoma ‘Chiki’ yeye alipoulizwa, alijibu: “Hakuna haja ya kuzushiana suala kama hilo maana ‘ngoma’ haina alama na kama hivyo basi wote tunayo, maana mtu yeyote anaweza kuamka na kusema hivyo, sijapenda na kwa staili hii sisi wasanii tunadhalilishana sana.”
Mwenyekiti Mstaafu wa Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’ alipoambiwa habari hizo, kwanza alishtuka kisha akafunguka:
”Jamani kuna mambo ya kuongelea lakini si uzushi kama huo, maana ni uchafu hata kumuandika mtu kwa tuhuma kama hizo sijapenda, huu uzushi unadhalilisha sana, binafsi nisingependa kuuongelea.”
Irene Uwoya, Makamu Mwenyekiti wa Bongo Movie hakupatikana hewani.
Picha na Global Publishers



No comments:
Post a Comment