HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » 'Mikopo ya elimu ya juu itolewe bila ubaguzi'


Baadhi  ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wametaka Katiba mpya iwe na kipengele ambacho kitaondoa matabaka katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Waliyasema hayo jana wakati wakitoa maoni ya katiba.

Juliana  Ng`onda,  alisema kama serikali inataka kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu ni vema katiba mpya ikaondoa kipengele cha kutoa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa kufuata ufaulu wao.

“Ninaomba katiba mpya itamke kwamba mikopo kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu isitolewe kwa kufuata ufaulu wao bali iwe inatolewa sawa kwa kila mwanafunzi mwenye sifa ya kujinga na elimu ya juu,” alisema.

Juma Hassan, alisema: “Endapo katiba  mpya itatamka hivyo, idadi kubwa ya wanafunzi hususani wanaotoka katika familia maskini watapata fursa ya kuendelea na masomo.”

Hassan  alisema asilimia kubwa ya wanafunzi wanaotoka katika familia duni hushindwa kuendelea na elimu ya juu  kutokana na kukosa ada.

“Wanafunzi wa wanaotoka katika familia duni wanasoma katika mazingira magumu sana, hivyo kupata alama ya juu ya kuwawezesha wapewe mkopo  kama wale wanaotoka katika familia  zenye uwezo mkubwa ambao wengi wao hufaulu vizuri,” alisema na kuongeza

“Sio rahisi, lakini ukifuatwa  utaratibu wa kutoa mikopo hiyo kufuatana na ufaulu,  watawakomboa.”

CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: