Redd's
Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred, ambaye yupo mjini Bukoba akikabidhi
sehemu ya misaada kwa Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Msingi,Mugeza
Mseto wakati alipotembelea Shule hiyo ambayo ni maalum kwa watoto wenye
ulemavu ya Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye ulemavu.Miss
Tanzania huyo pia alitembelea Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto
yatima kilichopo eneo la Kashai.
Redd's
Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred (katikati) akikabidhi mafuta maalu
ya kupaka watu wenye ulemavu wa Ngozi,kwa mmoja wa wanafunzi wa shule
hiyo.Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.
Mmoja
wa Watoto waosoma katika shule ya Mugeza Mseto iliopo mjini Bukoba
ambaye ni Mlemavu wa Macho akipokea fimbo maalum ya kutembelea.
Mrembo
Brigitte Alfred, ambaye pia ni Balozi wa Walemavu wa ngozi,
(Albinos) ametoa misaada ya kijamii katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni
pamoja na Fimbo maalum za kutembelea walemavu wasioona, Miwani, Kofia na
Madawa ya ngozi kwa ajili ya Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.
Redd's
Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu
wa ngozi anaeleleka katika kituo cha Kituo cha Nusura ambacho kinatunza
watoto yatima kilichopo eneo la Kashai,mjini Bukoba.Kulia ni Mkuu wa
Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.
Redd's
Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred akiwa kwenye picha ya pamoja na
baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma kwenye shule ya Mugeza Mseto
iliopo mjini Bukoba.
Kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam,Redd's Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli zingine za kijamii.
PICHA NA MICHUZI



No comments:
Post a Comment