Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Zahor Kassim Mohamed EL-KHAROUSY kuwa Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi katika Bahari Kuu.
Taarifa iliyotolewa na kutiwa saini leo,
Ijumaa, Desemba 7, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
inasema kuwa uteuzi wa Bwana El Kharousy ulianza Novemba 28, mwaka huu,
2012.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kharousy alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Desemba, 2012




No comments:
Post a Comment