Mshambuliaji
wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya
Zambia katika mchezo wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda goli 1-0.
Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
Mchezaji
wa timu ya Zambia, Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya
Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
Mchezaji
wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijipinda kumramba chenga Kiungo wa
Stars, Salum Abubakar, kutaka kumtoka wakati wa Mchezo wa Kirafiki wa
Kimataifa uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
Hii ni Nduki aliyoipiga Mrisho Ngassa
na kuingia wavuni moja kwa moja huku kipa wa timu ya Zambia Chipolopolo,
Danny Munyao akiwa hana la kufanya na kuishia kuutizama ukijaa wavuni.
Hili ndilo goli la Mrisho Ngassa , Mpira ukijaa wavuni
Baada ya kufunga goli alianza kwa kushangilia kwa namna hii kama anavyoonekana katika picha
Hii ni sehemu ya pili katika kushangilia
Sehemu ya tatu akipiga saluti yote hiyo ni katika mwendelezo wa kushangilia
Baada ya furaha aliamua kumbeba, Ari Kiemba badala ya kubebwa yeye
Mashabiki
wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars wakiwa na nyuso za furaha
baada ya Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Zambia.
Baada ya furaha aliamua kumbeba, Ari Kiemba badala ya kubebwa yeyeKatika
mchezo huo, Taifa stars imeibuka ushindi wa bao 1-0, lililotiwa kimiani
na Mshambuliaji machachaari, 'Kisirani' Mrisho Ngassa katika dakika ya
45 ya kipindi ca kwanza.
No comments:
Post a Comment