HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BREAKING NEWS: JENGO LA GHOLOFA LIMEPOROMOKA LOTE MAENEO YA BARABARA YA MOROGORO MTAA WA HINDIRA GHANDI, POSTA JIJINI DAR ES SALAAM

 
Taarifa lizizotufikia hivi punde zinasema kuna Jengo jipya lililokuwa linajengwa limeporomoka na kuangukia msikiti (kama inavyoonekana pichani) asubuhi hii mwendo wa saa mbili na nusu, katikati ya jiji la Dar es Salaam, kwenye barabara ya Mororogo. Kilicho kuwa kituo cha mabasi ya Sinza zamani uko posta, mtaa wa Hindi Ragani na yapata watu 60 takribani kuwa ndani ya poromoko ilo, na pamoja walio kuwa karibu ya jengo ,wakiwemo na hawa omba omba. Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 
Mtoto Maisamali Karim (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat iliyoangukiwa na jengo hilo.
  Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.

   
Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.

 
 Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova. 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni Mbunge wa viti maalum (NCCR-Mageuzi James Mbatia.
 BLOG YA PAMOJAPURE INATOA POLE KWA FAMILIA, NDUNGU NA JAMAA WALIOPATA AJARI HII

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: