Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar,
jirani na nyumba ya staa mwenzake, Wema Sepetu ambapo Wolper aliyekuwa
akiendesha gari lake aina ya Toyota-Brevis Saloon alivaana uso kwa uso
na gari lingine aina ya Toyota-Nadia.
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kwani hakuumia popote.
“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.
“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.

No comments:
Post a Comment