Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi Daraja la Suka Golani jijini
Dar es Salaam jana. Kushoto anayeangalia ni mbunge wa Ubungo-Chadema,
John Mnyika.(Picha na Freddy Maro-IKULU)
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akikata utepe kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es
Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dar es Salaam Bwana Madabida, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan
Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik, Meya wa
Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda na kulia ni Mbunge wa Ubungo-Chadema
Mhe. John Mnyika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ubungo-Chadema, John Mnyika wakati
alipokwenda kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akitembelea Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam jana.
Kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Yusuf
Mwenda na Mbunge wa Ubungo-Chadema John Mnyika.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waishio eneo la
Golani Kimara Suka muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani.
Wananchi wa vyama
mbalimbali vya Siasa wakishangilia wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa
akiwahutubia muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani jijini
Dar es Salaam jana mchana.



No comments:
Post a Comment