Wananchi wa Kisasa West Blk A wakiwashangaa mafundi waliokuwa kwenye nyumba ya Ivan Chibarangu kwa ajili ya ujenzi wa uzio na kuboibomoa bila ulinzi wa polisi wala kibari cha mahakama.
Ivan Chibarangu akionyesha ukuta wa uzio uliojengwa na mafundi wanaodaiwa kulipwa na Kimbinyiko na baadae kuibomoa nyumba yake.
Balozi
Rehema Mabwai akifuta machozi wakati alipokuwa akilalamikia nyumba yake
kuwa katika hatari ya kuvunjwa baada ya kuona ukuta wa uzio umejengwa
kuzunguka nyumba yake.
Mimea
ya mahindi ikiwa imeanguka kwa kukanyagwa wakati wa ujenzi wa uzio
uliozunguka nyumba tatu na wamiliki wake kutakiwa kuondoka na anayedaiwa
kuwa mmliki wa mabasi ya Kimbinyiko
Mmoja
wa Vibarua akipanga matofari nje ya njumba ya Salome Mabwai iliyo ndani
ya ukuta uanaodaiwa kujengwa na mafundi wa Kimbinyiko.(Picha na John Banda)
Na John Banda, Dodoma
KIMBINYIKO avamia nyumba za watu na
kuzizungushia uzio, huku akiwatisha wenye nyumba, kuwadharirisha, kuzibomoa na
kutumia polisi kuwasweka lupango wanapojaribu kudai haki zao.
Mmliki huyo wa Mabasi yaendayo
mikoani yenye jina la kampuni ya Kimbinyiko bila ya Hofu yoyote aliamua
kutekeleza adhima yake hiyo ya kuchimba msingi na kujenga uzio huo kwa siku
mbili akizungushia nyumba 3 alizozikuta huku watu wakiishi ndani yake.
Jumapili hii Mmiliki wa nyumba
mjawapo inayotazamana na Bwawa njiapanda ya Merriwa Manispaa ya Dodoma aliamua
kujaza watu kwa kuamua kupiga Filimbi ili apate msaada kutokana na nyumba yake kubomolewa
kwa kuvunjwa sehemu moja ya ukuta na Baadhi ya bati kung’olewa kwenye paa la
juu.
Wakiongea kwa masikitiko wamiliki wa nyumba
hizo Rehema Mabwai 58, Salome Mabwai 78, na Ivan Chibarangu walisema wanashangaa na kinachoendelea na hawajui cha
kufanya maana mwenye pesa aliamua kuwatesa hivyo kutokana na unyonge wao bila
kujali wao walifyeka na kujenga eneo hilo mwaka 1984 .
‘’Nimefika asubuhi nimekuta wamepanda
juuu wanabomoa nyumba yangu nikapiga Filimbi ili nipate msaada baada ya watu
kujaa wameacha lakini ona uhalibifu huu wa kubomoa sehemu ya ukuta na bati
walizong’oa, leo sitoki maana nikitoka kufuatilia Sheria wenzangu wanajenga
mpaka wamemaliza kuta za uzio’’, Alisema Chibarangu
Aidha Rehema Mabwai ambae pia ni
Balozi na mmiliki wa nyumba ya pili aliongeza kuwa Kimbinyiko alimuahidi kumjengea
nyumba ya vyumba viwili nje ya uzio atakapomaliza ujenzi wake na hivyo kuwataka
wasiwe na wasiwasi
Alisema wao hawajui Sheria wala kujua
pa kwenda kulalamika lakini wanaomba wasaidiwe ili wasiweze kupoteza haki zao
kutokana na wao kuishi ene hilo kwa muda mrefu sawa amesema atanijengea mimi je
mama ataenda wapi au nyumba yake haitambuliwi?
Kwa upande wake mmoja wa wapangaji 8
wa nyumba hiyo iliyoanza kubomolewa Valian kiona alisema wao ni wapangaji wa
nyumba hiyo kwa kipindi cha miaka 3 na kwamba Ivan Chibarangu ndiye
aliyewapangisha lakini wiki iliyopita alifika mtu ambaye hawakuwahi kumuona na
kuwambia yeye ndiye mwenye nyumba hiyo.
‘’Jana Jumamosi alikuja tena wakati
ujenzi wa uzio ukiendelea akatupa kila mpangaji 20,000 na kututaka tuhame
kuanzia jana bila kujua ni wapi tunaenda labda Barabara ya Isiza au kule
Bwawani na kila mtu akaondoka maana tuliogopa kupoteza vyombo vyetu kwa sababu
alituambia ataibomoa leo’’, alisema
Kwa upande wake mmiliki huyo wa
Mabasi ya Kimbinyiko alipotafutwa ili atoe ufafanuzi kuhusu tuhuma hizo
alishindwa kupatikana pamoja na juhudi kubwa alizofanya mwandishi wa habari hizi
aliyeshindwa kupewa ushirikiano na Fundi Juma Galan aliyewataka wananchi hao
kutosema chochote kwa madai ya yeye kulipwa hivyo asizuiliwe kufanya kazi yake
huku akikataa kusema lolote hata namba ya simu ya Bosi wake alikataa kutoa.
Hata hivyo ilibidi mwandishi atafute
Moja ya Tiketi Za mabasi hayo na alipopiga moja ya namba ilipokelewa na mtu
aliyejitamburisha kwa jina moja la Venus alipoelezwa alisema mkuu alikuwa
polisi anshuhulikia swala hilo maana alienda na polisi kumkamata mmoja wa hao
wenye nyumba.
Aliongeza kuwa angemjulisha bosi wake
au kutuma namba yake ya simu ambayo hata hivyo haikutumwa na hata alipopigiwa
tena alisema amuombe kibali cha kuitoa ndipo aitume lakini mpaka sasa
haikutumwa wala kujibu meseji aliyotumiwa.
Kamanda wa polisi David Misime
alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema Bado halijamfikia lakini atalifuatilia na
kwamba atahusisha mamlaka zinazohusika ili zithibitishe nani ni mmliki halali
wa eneo hilo ili Sheria itachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment