Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.
Askari anayedaiwa ni wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) anadaiwa
kuua dereva wa bajaj kwa kutumia bunduki katika maeneo ya Kawe Shoko,
jijini Dar es Salaam.
Tukio la kuuawa kwa kijana huyo jana jioni inadaiwa lilitokana na kutokea mabishano kati yake na mwanajeshi huyo wakati ikipita eneo ambalo raia hawaruhusiwi kupita.
Vurugu kubwa zilitokea katika eneo hilo baada ya kutio hilo huku vijana wenzake marehemu kukusanyika kuhoji sababu za kuawa kwa mwenzao.
Mashuhuda walisema kuwa baada ya askari kuho kumpiga risasi kijana huyo na kumuua, mwili wake ulichukuliwa na gari la kubebea wagonjwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Mwandishi wa NIPASHE alipofika eneo hilo majira ya saa 2:15 usiku, alikuta wananchi wakikimbia hovyo na huku milio ya risasi ikisikika.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, aluthibitisha alikiri kutokea kwa tukio na kuongeza kuwa bado Jeshi la Polisi linafuatilia ili kupata taarifa zaidi.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment