HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WAKILI NYAGA MAWALA AZIKWA LEO HUKO KENYA

Mwili wa marehemu Nyaga poul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa(Picha na Father Kidevu)
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akiwa kwenye mazishi ya wakili maarufu Nyaga Mawalla aliyefariki nchini Kenya.
Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema katikati akiwa kwenye mazishi ya wakili Nyaga Mawalla.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Buriani akiwa na mwanasheria maarufu Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya uwakili ya Law /Access Advocates Mosses Mahuna wakiwa nje ya kanisa la Lutherani nchini Kenya.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro wilani Simanjiro mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Laurence Marsha wakiwa kanisani nchini Kenya maziko ya marehemu Poul Mawalla.
 Sir George Kahama na mkewe wakiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Nyaga Mawalla.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Batilda Buriani akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Nyaga
 Jaji Mark bomani nae alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki mazishi hayo.
 Wanafamilia wakiweka mashada ya maua 
 
 Watoto wa Marehemu Nyaga wakiwa na ndugu zao. 

Mazishi ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Makampuni ya Mawalla ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi Kenya katia Makaburi ya Jumuia ya Langata.

Mapema kabla ya Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika Kanisa la KKKK, Uhuru Highway. 

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria Mazishi hayo ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama, Mwemyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria mabalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Marehemu Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwaa amelazwa kwa matibabu  Hospitali ya Nairobi.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: