HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » TIZAMA YALIYOJIRI KWENYE VURUGU ZILIZOTOKEA TUNDUMA LEO

 
Taarifa  kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai  kuwa hali  si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa  vurugu kubwa zinazodaiwa kusababisha na masuala ya  kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam .

Mwandishi   wa mtandao huu  kutoka Tunduma mkoani Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa  vurugu  hizo zimeanza  majira ya saa nne asubuhi  kwa makundi  ya vijana  kuandamana mitaani na kuvutana  kuhusu uamuzi  wa viongozi  wa dini ya kikristo Tunduma  kuandika barua kwa mkuu  wa wilaya  kutaka  kuruhusiwa kuchinja  wakati wa pasaka.

Alisema  kuwa kabla ya  ijumaa kuu  viongozi hao  wa dini ya Kikristo  walikutana na mkuu  wa  wilaya  ya Momba Abuud Saibea ambae  aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya  kufanya hivyo .

Hata hivyo inaelezwa  kuwa  vurugu  hizo za  leo hazina mahusiano ya moja kwa moja na masuala ya dini kwani  wanaoshiriki katika  vurugu  hizo ni vijana  wapiga debe ambao baadhi yao  wamechanganyika na  vibaka  kwa lengo la kuchafua hali ya hewa .

Kwani  suala la uchinjaji ambalo lilifanyika  siku ya Pasaka  halikuwa na mvutano  wowote baada ya wakristo kuchinja katika bucha zao na  waislamu hao  kuchinja katika mabucha yao na kila mmoja  kufanya biashara  kwa kupata  wateja wake kama kawaida .

Ila katika hali ya kushangaza ni baada ya  leo kuibuka  kundi hilo la  vijana  wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali kuanzisha vurugu kiasi cha  polisi  kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya  wananchi  waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali .

Kutokana na vurugu  hizo mpaka  wa Tunduma  ambao unaingia nchi  za kusini  wa Tanzania  ulifungwa  pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka  Sombawanga  pia  kuzuiwa  kuendelea na  safari hadi hali  hiyo  ilipotulia mida hii saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa  wa Mbeya  Diwani Athuman  kufika  eneo hilo.

Taarifa  zisizo rasmi ambazo bado kuthibitishwa na jeshi la polisi  zinadai kuwa mtu mmoja ndie amejeruhiwa japo hakuna madhara  makubwa  yaliyojitokeza .
 
 
HABARI NA FRANCIS GODWIN

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: