HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » SPIKA WA BUNGE ALAZIMIKA KUSITISHA SHUGHULI ZA BUNGE LEO KUTOKANA NA VURUGU ZILIZOTOKEA JANA MTWARA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.
Pia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini umesimamishwa kwa muda mpaka ufumbuzi wa tatizo la vurugu hizo utakapopatiwa suluhisho.

Kesho bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Afrika Mashariki itajadiliwa.
Taarifa ya serikali bungeni kuhusu vurugu zilizotokea Mtwarailisomwa na Nchimbi badala ya PM,
Chanzo kikuu cha vurugu ni kupinga gesi kusafirishwa kutoka Mtwara hadi Dar. Vurugu zilianza kwa kusambazwa vipeperushi vya kuhamasishana kufanya vurugu

Athari
Nyumba ya Mbunge imechomwa, ofisi za CCM kata, Nyumba na ofisi mbalimbali
watu 91 wamekatwa, hali hiyo imedhibitiwa jeshi la ulinzi limeenda kwa ombi la RC ambapo wakiwa njiani kuelekea huko askari 4 wamefariki kwa ajali ya gari
Nawapongeza askari waliofanya kazi katika mazingira magumu kurudisha hali ya amani

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: