Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumvamia Mbunge wa Kasulu



Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linawashikilia watu wawili , Jeremia Lawrent Mkude na Charles Chikumbili, kwa tuhuma za kumvamia na kumshambulia mbunge wa kasulu mjini kupitia NCCR - MAGEUZI mheshimiwa Moses Machali wakati anaelekea nyumbani kwake

Hayo yamesemwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. David Misime na kufafanua kuwa tukio hilo limetokea tarehe jana majira ya saa moja usiku katika eneo la area 'E' katika Manispaa ya Dodoma na kwamba baada ya msako mkali uliofanyika usiku wa manane watuhumiwa hao walikamatwa

Mheshimiwa Machali amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu

No comments

Powered by Blogger.