HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » PSG YATOA OFA YA PAUNI MILIONI 43 KWA CAVANNI

Mshambuliaji wa Napoli na Timu ya Taifa ya Uruguay, Edinson Cavanni


KLABU za Chelsea na Manchester City zitalazimika kuvunja rekodi ya dau la usajili Uingereza kama zinataka kumsaini mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavanni baada ya matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain kutoa ofa ya Pauni Milioni 43 kwa nyota huyo wa Uruguay. 

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini

Cavani anatakiwa na klabu zote, Chelsea na City, lakini dau la PSG linamaanisha watatakiwa kupanda ili kilipiku ndipo wampate mshambuliaji huyo.

Dau la PSG linakaribia Pauni Milioni 53.9, ambazo Napoli inataka ambazo zitahusu pia kodi wa dili hilo.
Real Madrid bado haijafika bei na Cavani alisema wiki iliyopita kwamba tetesi zimezidi kuhusu hatima yake. 

"Mwanzoni mwa Kombe la Mabara, sikuamini kwamba tetesi za usajili zingenisababishia matatizo. Lakini, mwishoni, nakubali wananisumbua kidogo,"alisema.

Chelsea inashikilia rekodi ya kusajili kwa bei chafu Uingereza, Pauni Milioni 50 walizotoa kumsaini Fernando Torres, Januari 2011.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: