Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush wakiwa kwenye makaburi ya waanga wa mabomu leo
Rais wa Marekani Barack Obama ameweka mauwa kwenye
makaburi ya waathiriwa wa mashambulizi ya mabomu dhidi ya ubalozi wa
Marekani nchini Tanzania mwaka 1998, kama ishara ya kuwakumbuka.
Raia 11 wamarekani waliuawa katika shambulizi
hilo lililofanywa na kundi la kigaidi la al-Qaeda ambaklo lilifanyika
wakati mmoja na shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani
mjini Nairobi, Kenya.
Obama aliuungana na rais mstaafu wa Marekani George W Bush kwa kumbukumbu hizo.
Rais Obama yuko katika mkondo wa mwisho wa ziara yake ya pili ya Afrika akiwa rais , ambapo alitembelea Senegal na Afrika Kusini.
Rais Obama yuko katika mkondo wa mwisho wa ziara yake ya pili ya Afrika akiwa rais , ambapo alitembelea Senegal na Afrika Kusini.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Aidha Obama pia atamtembelea kituo cha
kuzalishha umeme kinachomilikiwa na Marekani nchini humo, kufuatia
tangazo lake mwishoni mwa wiki la mradi wa umeme utakaogharimu mabilioni
ya dola.Mradi huo wa miaka mitano, unatarajiwa kusaidia kuongeza kasi ya uzalishaji wa umeme kusini mwa jangwa la Sahara,kwa ushirikiano na mataifa ya kiafrika pamoja na sekta binafsi.
Akiwa nchini humo, Obama pia anatarajiwa kuzindua mpango unaonuia kusaidia nchi za Afrika Mashariki ikiwemo, Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda kushirikiana kibiashara.
Wakati huohuo, mkewe Obama, Michelle anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa wake za marais, unaoandaliwa na taasisi ya George W Bush huku ukiongozwa na mkewe Laura Bush.
SOURCE: BBC SWAHILI




No comments:
Post a Comment