HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » TIZAMA YANAYOENDELEA KUJIRI KWENYE MAONESHO YA SABASABA MKOANI DAR ES SALAAM

 Gari la Mbao lililoko kwenye banda la Utalii limekuwa kivutio kikubwa kwenye maonesho ya sabasaba

 Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakilitazama gari la mbao ambalo lipo katika banda la Maliasili na Utalii katika Maonyesho ya Sabasaba ambayo yanaendelea katika viwanja hivyo barabara ya kilwa
Muonekano wa Gari hilo la Mbao
 Muonekano wa Mbele wa gari hilo la Mbao lililopo katika Banda la Maliasili na Utalii


Endelea kutizama matukio kwa kubofya hapa chini


Wakazi wa Jiji la Dar Na vitongoji vyake wakilitizama gari lililotengenezwa na Mbao katika Maonyesho ya Sabasaba ambapo gari hilo lipo katika Banda la Maliasili na Utalii

..........................................................................................................

NMB ChapChap Acount yawa kivutio kikubwa kwenye maonesho ya Sabasaba

 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiwahudumia wateja waliofika katika Banda la benki ya NMB lililopo katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap ambapo mteja ufunguliwa akaunti yake papo hapo na kupewa kadi ya kutolea pesa kwenye mashine muda huo huo.
 Baadhi ya Wateja waliofurika katika moja ya gazebo la NMB lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB  katika Viwanja Vya Sabasaba wakifunguliwa akaunti ya ChapChap ambayo mteja ufunguliwa akaunti hiyo akiwa na kitambulisho cha kupigia kura na kupewa kadi yake ya kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo na kwa gharama ya Shilingi Elfu kumi tu
 Wateja waliofika katika Moja ya gazebo lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB katika viwanja vya sabasaba wakipata maelezo mara baada ya kufungua akaunti zao za ChapChap na kukabidhiwa kadi zao za kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo kwa gharama nafuu ya shilingi Elfu Kumi tu.
 Afisa mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Bw Respecious Denis akitoa maelezo ya akaunti ya Chapchap kwa Mteja aliyemaliza kufungua akaunti hiyo mara baada ya kufika kwenye moja ya gazebo la Benki ya NMB lililopo katika Viwanja Vya sabasaba mapema leo
 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiwahudumia wateja waliofika katika gazebo la Benki ya NMB lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB kwaajili ya Kufungua akaunti ya Chapchap ambapo mteja akimaliza kufunguliwa akaunti ukabidhiwa kadi yake ya kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo
 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiendelea na zoezi la kuwafungulia akaunti ya Chapchap wateja waliofika katika moja ya gazebo la Benki ya NMB kwaajili ya kufungua akaunti  ya Chapchap Kulia Ni baadhi ya Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakijiandaa kwaajili ya kumpiga Picha mteja aliyefika kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap.
 Afisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Maana Katuli akimpiga picha mteja aliyefika katika Banda la NMB kwaajili ya Kufungua Akaunti ya Chapchap ambapo mteja akimaliza kufunguliwa akaunti anakabidhiwa na kadi yake ya kutolea pesa papo hapo
 Wateja wakipata maelezo ya kutosha kutoka Kwa Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB
 Mteja akichukuliwa alama za vidole na mmoja kati ya maafisa mauzo ya nje wa benki ya NMB waliokuwa wakimuhudumia wakati mteja huyo alipofika kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap
Afisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Batuli Suna akichukua alama za vidole vya mteja alifika katika banda la benki ya NMB kwaajili ya Kufungua akaunti ya Chapchap katika Maonyesho ya 37 ya Kibiashara ya Kimataifa

.....................................................................................................

Huu ndio mwonekano wa Smile Communication kwenye viwanja vya Sabasaba



 Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Smile Wauzaji wa Router kwaajili ya matumizi ya intaneti akiwa na tabasamu la nguvu kama jina la kampuni anayoifanyia kazi katika banda lao lililopo katika Viwanja Vya Sabasaba
 Bwa Deogratias Kabeho, Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Smile (Wa kwanza Kushoto) akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake katika banda lao lililopo Katika Viwanja Vya Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.
 Wafanyakazi wa Smile wakiwahudumia wateja waliofika katika banda lao kwaajili ya kupata maelezo juu ya kufungiwa router za smile ambazo zina spidi ya hali juu kabisa kuliko mitandao mingine ya intanet hapa nchini,nyuma yao ni runninga inayoonyesha video za muziki unaochezwa katika laptop iliyounganishwa na intanet ya Smile yenye Spidi ya 4G LTE
Wafanyakazi wa Kampuni ya Smile inayohusika na ufungaji na uuzaji wa router za intanet zenye spidi ya 4G LTE wakimuelekeza mteja wao aliyefika katika banda lao lililopo katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kupata huduma ya kufungiwa intanet na kampuni ya Smile ambayo ina spidi ya hali ya juu ya 4G LTE.


PICHA NA JOSEPHAT LUKAZA WA LUKAZA BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: