Vijana wengi wa kiume hujikuta katika wakati mgumu kuchukua maamuzi ya kuishi na mwanamke japo yawezekana wakawa wanatamani kufanya hivyo kwa muda mrefu kutokana na vikinza vingi, vingine vikiwa ni vya kimaisha na vingine ni nadharia tu.
Katika bandiko hili, nitagusia sababu kadhaa zinazochangia vijana wengi kujikuta wakisuasua au kuogopa kuingia kwenye ndoa.
Kupanda kwa gharama za maisha
Kigezo hiki huwakumba zaidi wanaume ambao wanaishi mijini. Gharama za maisha zimepanda sana kiasi kwamba mtu anaweza kuwa anaishi peke yake na bado kuna mambo ambayo anashindwa kuyatimiza kwa wakati, kama vile kozi ya nyumba, pesa ya kujikimu na mengine mengi. Wengi huona ni heri kuwa na mtu tu ambaye ni mpenzi wake kuliko kudhibiti kabisa kwa kuwa na huyo mtu kwa kuishi naye kwa hofu ya kushindwa kutimiza wajibu. Ndio maana kwa wale ambao hupata akina dada ambao wanajiweza kujitegemea na hivyo ni hodari kwa kusaidiana katika mambo ya kila siku hasa katika masuala ya maendeleo huwa wepesi kuchukua maamuzi ya kuoa.
Utitiri wa wanawake wanaopatikana kirahisi bila hata kuoa
Ni suala ambalo lipo wazi hasa maeneo ya mijini akina dada/mama wa kuwa nao katika mahusiano (bila kujalisha ni wa muda mfupi ama mrefu) wamekuwa wengi, rahisi kuwapata, wa kila aina mwanaume watakao. Kuna wanaume wamejikita katika hilo kiasi kwamba mradi tu atake mwanamke atatoka/atatumia namba alizohifadhi kwenye simu na atafanikisha hiyo azima yake ndani ya siku hiyo hiyo ambayo amedhamiria bila shida yoyote. Hii inafanya kwa kiasi kuchangia kwa wanaume kusuasua katika maamuzi ya kuoa. Kwa kimombo hujiambia, “If I can get it for free, why buy it?”
Maradhi hasa ugonjwa wa UKIMWI
Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDs kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto. Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa. Naomba izingatiwe kuwa si wote; wengine huwa hodari na huoa/olewa saa nyingine bila hata kumjulisha mpenzi wake huyo kuwa yeye ana virusi chanya vya UKIMWI (HIV +ve).
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Kufurahia ‘uhuru’
Hawa ni makapera wazoefu (wengine husema ‘bachela sugu’), hakuna mtu ambaye anaweza mshawishi akabadilisha maisha yake hayo ya kikapela (bachelor). Miaka huzidi kukatika hadi anafika miaka takribani 40 au zaidi wala hana mpango wa kuoa na wala hajutii maamuzi yake hayo. Mara nyingi wanaume wa namna hii hupenda sana wanawake (siyo lazima kuwa atawachanganya kwa kuwa na zaidi ya mmoja); huwa na uwezo (hata kama sustainable); Hutaka wanawake wadogo (mtu mzima sana kwake hapana hata kama yeye ni mtu mzima); Ni mtu wa starehe sana, haoi kamwe na hufurahia uhuru huo kwa hisia kuwa akioa ataupoteza uhuru wake.
Uhaba wa wanawake wanaofaa kuolewa
Na hii hutokea hasa kwa maeneo ya mijini. Wadada/mama wengi wamekuwa ni ‘wa mjini’ mno, wajanja, malengo mbele ikiwa imeambatana na tamaa, wanaoweka pesa mbele utu nyuma, wachanganyi (kuwa na bwana zaidi ya mmoja). Haya mambo yamekuwa yakifanywa bila kificho, inamfanya mwanaume anapokuwa katika mahusiano ahisi kuwa hata mtu wake ana tabia hizo hizo hata kama siyo kweli. Hii inakatisha tamaa kwa wanaume wengi na kuona wanawake wanaofaa kuoa (tokana na viwango vyake alivyoweka) ni adimu ama hawapo kabisa!
Kutopata ampendaye kwa dhati
Kuna wanaume vigezo vya mwanamke awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuoa. Yeye kikubwa anataka ampate mwamake ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mwanamke atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanaume anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mkewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanamke akampenda. Kama huyo mwanamke atakubali kuolewa ama lah; hilo ni suala jingine!
Mahusiano mabovu ya awali
Kuna wanaume huchagua wanawake kwa sifa ambazo anazijua yeye mwenyewe. Yeye hamuangalii mwanamke kama mtu, bali anamuangalia kama kitu. Daima vigezo vyake ni nataka mwanamke wa hivi, tabia za vile, muonekano wa kule na mambo mengine kedekede. Hivyo unakuta kila siku yuko katika mahusiano na mwanamke ambaye ni kweli anampenda kimuonekano; ila linapokuja suala la tabia wanashindwana kabisa. Anaachana nae kisha anatafuta mwingine kwa mtindo uleule – mwisho wa siku analaumu wanawake wote ni sawa na kukata tamaa ya kuoa ama kusuasua katika maamuzi ya kutaka kuoa.
Kutoridhika na kipato chake
Kuna mwingine anaweza kuona kutoridhika na kipato (ni sawa na sababu ya kwanza niliweka ya “Kupanda kwa gharama za Maisha”) – lakini hii ni tofauti kidogo. Hapa namaanisha pale ambapo mwanaume ana uwezo kabisa wa kuwa na mke na pia kuweza kukimu mahitaji yote pamoja na ya familia yake. ILA kwa mipangilio yake anaona yeye bado; mara nyingi wa hivi anataka ahakikishe ana uwezo wa kutosha ili aweze kuishi maisha ya kifahari na si ya kujitosheleza tu. Hivyo katika hali ya kawaida ana uwezo wa kuwa na mke lakini kwa maisha ya mtu wa kawaida na si wa kitajiri kama malengo yake.
Malezi na Makuzi
Dhana mbovu juu ya ndoa
Dhana ya ndoa inaenda ikibadilika… Kumekuwa na tabia ya watu kukatisha tamaa kwa kutoa vigezo, sababu, hadithi juu ya ndoa ambazo ni za kubomoa kuliko kujenga. Sijui hawa watu hutumia vigezo gani… HATA siku moja usitarajie uishi na mtu miaka nenda miaka rudi kitanda kimoja, nyumba moja msigombane, kusiwe na madhaifu na pia kusiwe na wakati ambao wote hadi kiwango cha kukata tamaa. Ndoa ni zaidi ya starehe na kufurahi… Inahitaji nguvu kubwa, nguvu ya ziada, hekima, busara, kujituma na pia kuwa committed kwa ndoa kuweza kufanikiwa. Sisemi kuwa lazima zote zitafanikiwa maana kuna mambo ambayo yana mpaka – kuna wakati you just let go. Ila hakuna haja ya kuibomoa hiyo taasisi kwa makusudi, taasisi ambayo ni msingi bora wa malezi ya watoto kuliko taasisi yoyote ile inayoweza lea watoto ambao hasa ndiyo tegemeo la vizazi vijavyo.
Kuzaa ovyo/Kuzaa kabla ya ndoa
Kuna wanaume wanazalisha balaa! Bila kujalisha hizo mimba ni zao kweli ama wamesingiziwa kinachojalisha na watoto hao kawakubali na anawalea. Kuna wanaume hadi anafikia umri wa miaka 30 tayari ana watoto wa wanawake tofauti hata watano na analea. Kwa kiasi fulani, hii inaweza mvunja morali ya kutaka kuoa, anaona kama watoto tayari anao na anawalea hivyo hakuna haja ya kuwa na mwanamke kabisa ndani kama mke. Hii ni mara chache.
Kukua kwa idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa
Maadili mengi ya wanandoa yamezidi kushuka… Hapo nyuma ilishazoeleka wanaume huwa na tabia ya kutoka nje ya ndoa na wanawake kwa uchache. Bahati mbaya siku zinavyozidi kwenda idadi ya wanawake wanaotoka nayo inakuwa kwa kasi, tabia ambayo inafanywa bila kificho kabisa na imekuwa kana kwamba ni mashindano ya kutoka. Ni wazi thamani (reputation) ya mwanamke ambaye anatoka na mwanaume anayetoka ni tofauti. Ni wanaume wachache wana kifua cha kuweza kuvumilia mkewe/mpenziwe kutoka nje na kuendelea kuwa naye. Kwa wanaume wengi ambao hawajaoa hili huchangia katika kukata tamaa ya kupata mwanamke ambae anafaa kuwa mke na asiyeweza kuwa msaliti.
CHANZO: FIKRA PEVU
No comments:
Post a Comment