Abiria wakiwa tayali wameshuka katika Daladala baada ya kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma na kushushiwa Barabarani baada ya kukuta msongamano mkubwa katika stand mpya iliyoanza kutumika leo ya jamatini.(PICHA NA JOHN BANDA, DODOMA)
Mmoja wa viongozi wa wafanyabiashara Ndogondogo Danny Msitewa akifafanua jambo alipokuwa akisoma majina na kuwapa namba za utamburisho wa nafasi za kuweka vibanda vyao katika stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma
Wafanya biashara waliokuwa stend iliyokuwa ya muda ya daladala oil com wakikusanya bidhaa zao zilizosambazwa na tingatinga lililofika kubomoa vibanda walivyokuwa wakaifaanyia biashara zao ili kuwashinikiza kuondoka eneo hilo.
Endelea kusoma habari hii kwa kuboya hapa chini
Asikari akitoa maelekezo kwa baadhi ya watu waliokuwa wakivizia kukwapua mali za watu zilizozagaa stand ya Daladala ya oil com Baada ya kubomolewa vibanda vyao ili wahame katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Mipango miji na Mazingira manispaa ya Dodoma Stephen Mwanga akiwatangazia wafanya biashara ndogondpgo kutoendelea na ujenzi mpaka baazi ya taratibu zitakapokamilishwa.
Msukuma Tololi akiingiza moja ya vibanda vya wafanyabiashara katika Stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma iliyoanza kutumika leo
Magali ya Daladala yakisubili abiria ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
Daladala zikisubili kuingia ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
Kazi ya bomoa bomoa ikiendelea stend ya mkoa
Na John Banda, Dodoma
MWENYEKITI wa kamati ya Mipango miji na
Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi wa
vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya
Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.
Machinga hao wamesimamishwa kujenga
siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya kufungwa
mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya watumiaji
wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.
Mwenyekiti huyo aliwataka kusimamisha
zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana na kile
alichosema ugawaji ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu kutokana na
viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.
Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo hilo
kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia
kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi
wao walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi
huo haujaanza Augost 2012.
Alisema alipofika na kujionea
kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali
halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda
lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa
manispaa ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.
'' Nimesimamisha ujezi usiendelee kwa
sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu
ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa
manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'',
alisema Mwanga
kwa upande wao baadhi ya Machinga hao
walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia
majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa
hata wakati staend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi
hizo zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao
wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi
kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa
tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya
katika ugawaji.
TATIZO LA UDOGO WA STEND LAIBUKA
WAKAZI wa manispaa ya Dodoma
wamelalamikia udogo wa Stand kuu ya Daladala ya Jamatini na kuitaka
mamlaka nayohusika kuliacha eneo la oil com zilikokuwa zikipakilia
abiria wakati wa ujenzi wa stand hiyo kuwa mbadala kutokana na wingi
wa magali.
Kauli hiyo ilitolewa wakati stendi hiyo
ilipoanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza jana ambapo ilishuhudiwa
wingi wa magali hayo ya Abaria yakiingia na kutoka huku kukiwa na
msongamano mkuwa kiasi cha mengine kushushia abiria Barabarani.
Mmoja wa Abiria wanaotumia stand hiyo
Winnie Binamu alisema imejengwa vizuri lakini haikidhi haja kutokana
na kuwa ndogo ukilinganisha na idadi kubwa ya Daladala zilizopo hali
inayosababisha msongamano na wengi kushusha abiria bila utaratibu
ilimradi wawahi kupakia wengine.
Winnie aliongeza kuwa niafadhali kama
wahusika wangeiacha stand iliyokuwa ikitumika kwa muda ya oili com
kuendelea kutumiwa na baadhi ya magali ya njia nyingine na mengine
kupelekwa jamatini kwa sababu kwa sasa watu ni wengi tofauti na
miaka ya nyuma.
Kwa upande wao madereva wa Daladala
hizi walisema stand pamoja na uzuri haikidha kutokana na njia moja
kuwa na magali zaidi ya 50 wakitolea mfano njia ya Chang'ombe,
Mipango, UDOM, na kisasa zenye abiria na Magali Mengi.
Mmoja wa madereva wa Daladala
zinazoelekea Ipagala Moses Mamba alisema kwa sasa Dodoma inawatu
Wengi walioletelezwa na vyuo pamaja na taasisi zilizo na zisizo za
kiserekali zinazoendelea kuhamia mkoani hapa hivyo ni vyema swala la
stand hiyo kuangaliwa upya na ikibidi iwekwe ya ziada.
'' Ona ndugu mwandishi leo ni siku ya
kwanza stand hii kuanza kutumika lakini msongamano ni kama unavyoona
wengi wanashushia abaria barabarani kuanzia hapa yanapoingilia maka
karibu na kipita shoto[ Round About] cha stand ya mabasi ya mkoani je
wakija wote kutokana na tunavyojua itakuwaje?'', Alihoji Mamba
Katibu wa Umoja wa wenye Daladala
[UWEDO] Peter Kabome alisema Stendi hiyo haijawa Rasmi ni kama
inafanyiwa majaribio kwa sababu haiwezekanai yakatakiwa kuingizwa
magali zaidi ya 300 kwenye eneo linalochukua magali yasiyozidi 100.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango
Miji na Mazingira manispaa Stephen Mwanga alisema ameona msongamano
huo jinsi ulivyo mkubwa hivyo atahakikisha anavihusisha vyombo
vinavyohusika kikiwemo SAMATRA ili waweze kuona nini cha kufanya ili
walau kuliweka sawa la staend hiyo.
PICHA NA HABARI NI KWA HISANI YA JOHN BANDA, DODOMA
No comments:
Post a Comment