Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliomalizika kwa bao 3-3 kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mashabiki wa Simba, walikuwa kama wamemwagiwa maji, wakiwa na huzuni katika kipindi cha kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katika
mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3, ambapo Yanga ilipata
mabao yake katika kipindi cha kwanza kupitia kwa wachezaji Mrisho Ngasa,
aliyetupia katika dakika ya 15, Hamis Kiiza 36 na 45.
Mabao
ya Simba yalifungwa kipindi cha pili kupitia wachezaji wake, Betram
Mwombeki, katika dakika ya 54, Joseph Owino katika dakika ya 57 na
Gilbert Kaze, katika dakika ya 83.
Baada
ya Simba kusawazisha mabao yote matatu viongozi na mashabiki wa timu
hiyo walionekana kushangilia sare hiyo, ambayo kila mmoja aliyekuwapo
uwanjani hapo hakuweza kuamini kilichotokea kuanzia mashabiki, wachezaji
wa Yanga na hata wa Simba.
Mshambuliaji Mrisho Ngasa, (kulia) akimtoka beki wa Simba, Joseph Owino, katika kipindi cha pili.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba, Joseph Owino na Gilbert Kaze, katika kipindi cha kwanza.
Mrisho Ngasa, akiruka kwanja la beki, Gilbert Kaze.
Mashabiki wa Yanga ilikuwa ni furaha kama hivi, ambapo baadaye furaha hii ilizimika ghafla.
Katika mtanange huo, mashabiki kadhaa walizimia, ambapo shabiki huyu wa Yanga, akibebwa kutoka jukwaani baada ya kuzimia, huku mashabiki saba wa Simba na wawili wa Yanga walizimia.
Mshabiki wa Simba walizinduka na kushangweka kama hivi, baada ya kupata bao la pili.
Picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto Blog











No comments:
Post a Comment