Nguli wa muziki wa jazz nchini Kenya, Joseph Hellon,
ameuponda utaratibu mpya unaotumika kwenye shindano la Tusker Project
Fame msimu wa sita wa kualika waongozaji wa muziki wapya kila wiki.
"Unawezaje kumchukua msanii wa rap awafundishe waimbaji? Namheshimu
Muthoni the Drummer Queen lakini naamini angewatendea haki mashabiki
zaidi ya kuongelea kuhusu ujasiriamali. Aliwafanya waimbaji warap na
bado kwenye usahili unakuwa ‘disqualified’ kwa sababu hiyohiyo," alisema
Hellon.
ENDELEA KUSOMA HANBARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Amemponda pia Eric Wainaina ambaye ni principal kwenye academy kwa kusema:
Eric ni mtu anayeheshimika lakini anaonekana kupotea. Yupo hewani
anaimba ‘happy birthday’ na kuigiza lafudhi. Anatakiwa kuonesha uwezo
wake wa uongozi na kugawa maarifa yake. Sijaona maendeleo yoyote ya
sauti na uwezo tangu washiriki wajiunge na academy."
Wiki iliyopita rapper wa Muthoni the Drummer Queen alikuwa muongozaji
mkuu wa muziki kwa washiriki wa TPF6 na kabla ya hapo alikuwa Hermy B.




No comments:
Post a Comment