HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » HII NDIO PETE AINA YA SMARTY RING INAYOUNGANISHWA NA SMARTPHONE KWA BLUETOOTH, INAUWEZO WA KUPOKEA SIMU, NA KUTUMIKA KAMA REMOTE CONTROL

‘Smarty Ring’, ni pete inayounganishwa na smartphone kwa bluetooth, na kumuwezesha mtumiaji ku-control simu yake hata ikiwa mbali na yeye.
 Pamoja na kuwepo Smartwatches sokoni, sasa kuna pete inayoweza kuunganishwa na smartphone na kutoa taarifa (notification) pindi ujumbe, barua pepe, zinapoingia katika simu.
Ina buttons zinazoweza kutumika kupokea simu, na kuplay muziki uliopo katika smartphone ya mtumiaji.
LED screen ya pete hiyo huwaka pindi mtu aliyeivaa anapopokea e-mail, ujumbe mfupi, facebook na twitter notification, au simu inapoingia, na pete hiyo inaweza pia kutumika kama remote control.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Smarty Ring imebuniwa na engineer Ashok Kumar kutoka Chennai, India.
Pete hiyo imetengenezwa na ‘Bluetooth 4.0 sensor’ inayoweza kuunganishwa na simu yoyote ya Android au iOS kupitia application maalum ya Smarty Ring.
Panapokuwa hakuna notification yoyote kwenye simu, LED screen ya pete hiyo inaonesha muda.
Simu inapoingia, aliyeivaa pete anauwezo wa kuchagua kupokea au kuikata simu kwa kutumia buttons ambazo ziko pembeni mwa pete hiyo.

Smarty Ring zitapatikana kwa gharama ya $275 (442,000 Tshs) pindi zitakapoingia sokoni April mwakani.
Mwezi September wabunifu wengine wa Hungary walitambulisha pete kama hiyo ‘Ring Clock’, ambayo yenyewe inaonesha muda pekeyake.

SOURCE: MAIL ONLINE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: