HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAWAZO HUZAA UKWELI; VIJANA MPO? SOMENI HII! KISHA JITAMBUE


 Kijana mdogo wa sasa anawaza kula bata, sijui wana maana  gani bata ukimuangalia ni mchafu 
mawazo  yake ya ajabu ajabu fuatilia utaona. Siku hizi fasheni kuwa shabiki wa chama au 
timu inayofanya  vizuri kuliko kuyatafuta hayo mazuri ili tuwe na  maendeleo.  Na 
unamkashifu kabisa mwenzako kisa timu yako imeshinda jana, au chama chaka unaona
 ndio kinajua kuliko kingine, hivi kwanini tusioneshane umwamba kwa kuwa hata na fire
extinguisher katika nyumba zetu za kupanga au tulizojenga? Kwanini usituite vijana 
wenzako tuje shambani kwako kununua mananasi yaliyokuzidi kwa wingi ili upate fedha
 na sie tupate mananasi, ni mtazamo tu lakini kuna mengine mengi.
Katika maisha yangu hadi nimefikia umri huu nawaza kuwa na hotel ndogo tu hata isiwe
 na vyumba vingi lakini nashindwa  kwa kuwa sikuwa na mipango iliyo na umakini, miaka 40 
nawaza tu niwe na hiki niwe na kile.  Lakini unakuta kijana mdogo wa miaka 26 tu akiwa 
anamiliki hotel  yenye akili ingawa si kubwa sana lakini unamuona kabisa kwamba ni mtu 
anayewaza na wazo lake limezaa. Angalia hotel yenyewe ninayokuambia halafu utaniambia
 ninachozungumza. 
 
 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA 
HAPA CHINI
Napenda sana kuona vijana tukiwa na maendeleo, tena maendeleo ya kutolea jasho la njia 
ya halali na si njia za panya kama wengi tunaoona na kusikia kuwa wamekamatwa, 
wamefungwa, wameharibika akili na miili.
Huu ni wakati wa mabadiliko ya fikra na si kukaa chini na kuanza kulia kuwa wachina, sijui 
wawekezaji wanje wanachukua nafasi zetu, tupambane kuweza kujiingizia vipato kwa 
kuwekeza mawazo yetu, mitaji yetu, akili zetu, fedha zetu na uaminifu wetu katika shughuli 
za maendeleo ya kifamilia hadi kitaifa. Maendeleo hayaji kwa kuaihidiwa na baba,
 mama, kaka, mwanasiasa. Maendeleo yanakuja pale wewe unapozaliwa tu, umeletwa
 kwa kusudi maalumu na si kukaa kijiweni au barazani na kunyoosha miguu kama mikia ya paka
 huku unalalamika Fulani hafanyi hili, Fulani hafanyi lile.  Tukimchagua Fulani ndio ataweza,
 aisee unajidanganya ndugu yangu.  Ukitaka kuamini hilo wewe endelea kukaa na kulalamika 
na kuchagua viongozi wa kukupa maendeleo ndio utanielewa. Napenda kumpongeza kijana
 huyu kwa kutumia mawazo yake, ndoto yake, ubunifu wake, na kufikia hapo kwa njia sahihi 
aliyotumia.  Napenda kumuambia kuwa “ Napenda maendeleo yako, ila utanisamehe natamani 
kukuzidi”
 
Nikipata ruhusa nitaongea naye na atatufundisha njia alizotumia kufikia hapo alipo, vijana ni 
wakati wetu huu sasa kubuni na kuiga mema yatakayotufanya tuwe matajiri kwa njia sahihi. 
Nipo tayari muda wowote kuchangia mawazo ukiniomba katika mambo yenye tija na si 
kuniletea hadithina ulalamishi.  Nipo tayari kuwa na rafiki mmoja muelewa kuliko 100
wabovu, jifunze kutoka kwa walio endelea ili nawe uendelee.

Imeandaliwa na Buberwa Robert 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: