Wananchi wakiushuhudia mwili wa Juma Mbega ukiwa kwenye maji.
Kwa mujibu wa polisi, mwili wa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Juma Mbega (46) ulikutwa kwenye kichaka ukiwa umeharibika vibaya na kutoa harufu kali huku ukizungukwa na wadudu, nusura polisi wenyewe watoke nduki.
Wananchi wakiuopoa mwili wa Juma Mbega kutoka kwenye maji.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Morogoro, Afande Suzy alisema wakiwa ofisini, walisikia harufu kali
hivyo kulazimika kufanya uchunguzi ndani na nje ya jengo hilo la polisi
lenye ghorofa moja ambapo chini zipo ofisi za Jeshi la Polisi Wilaya ya
Morogoro Mjini na juu za mkoa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Simanzi baada ya kifo cha Mbega.
“Baada
ya kuchunguza harufu hiyo, tulibaini uwepo wa maiti kwenye kichaka
kilichopo nje ya ofisi zetu ambapo mwili huo unaokadiriwa kuwepo hapo
kwa zaidi ya wiki moja ulikuwa umeharibika vibaya na kutoa harufu kali,”
alisema afisa huyo.
Kwa
upande wake, Nuru Adam ambaye ni mjomba wa marehemu huyo, akizungumza
na gazeti hili eneo hilo la tukio alisema: “Huyu ni mjomba’ngu,
amezaliwa tumbo moja na mama yangu mzazi, Kilegu Hamis.
“Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka hivyo huenda alikutwa na matatizo hayo akiwa eneo hili peke yake.”
Baada ya uchunguzi wa awali na ndugu wa marehemu kujulikana, maiti ilichukuliwa na kupelekwa mochwari kuhifadhiwa huku taratibu za mazishi kwa ndugu zikiendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
na GPL
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
na GPL
No comments:
Post a Comment