HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » JINSI TAMAA ITAKAVYOKUFANYA UTAPELIWE KIRAHISI


Maisha yanasonga kwa kasi sana na vitu vingi vinatokea , lakini tamaa imekuwa ikibadilisha mwelekeo wa mtu kimaisha. Watu wengi wamekuwa wakitaka maisha fulani au vitu fulani ili waonekane ni watu wa maisha fulani. Unahitaji kuwa makini na kitu unachofanya hasa unachotamani kufanya. Tunaishi kwenye dunia ambayo inawezekana wazazi wetu hawakuishi hivyo hawana ushauri wa kutupatia katika maisha haya. Wewe ndio dereva unatakiwa kujifunza barabara mpya ambayo hakuna mtu alishawahi kupita.
Tamaa imekuwa ikitufanya tutamani maisha fulani ambayo kiuhalisia hatuna hivyo kutusababishia kufanya kila linalowezekana ili tufikie vitu fulani. Sasa katika hali ya kufanya kila linalowezekana, kuna watu wako kati ya tamaa zako na wewe mwenyewe ili watengeneze kitu hapo. Si mara zote marafiki zetu hutuambia ukweli, mazingira tuliyopo hakuna anayetaka kuambiwa ukweli hivyo unaachwa mpaka uharibikiwe ndio watu waanze tulijua unapotea n.k.
Kuna vitu kadha wa kadha kwenye tamaa ambavyo vinaendelea sasa ambayo unatakiwa kuvijua; 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI 

Utapeli wa Kwenye Mtandao;
Kuna watu wamekuwa wakituma barua pepe au sms kwamba umeshinda kiasi kadhaa cha fedha hivyo wanakuhitaji ukamilize baadhi ya hatua kwa kuwajibu na waendelee kutoa maelekezo zaidi. Kwa mtu mwenye akili timamu unatakiwa kujiuliza, je mimi nimeshiriki shindano lolote? Je unashindaje kwenye shindano ambalo hujashiriki? Kwa sababu ya tamaa zako binafsi unajikuta unaingia kwenye mtego, halafu unatapeliwa na wakikutapeli unakaa kimya hata humwambii mtu. Fanya Kazi na uache ndoto za alinacha!

Uasherati au Uzinzi;
Kila mtu anatapeliwa kulingana na udhaifu wake ulipo, kama wewe ni mzinzi au mwasherati kwenye facebook watu wamegundua hasa matapeli huweka picha nzuri ya mrembo ambaye ataomba urafiki kwako na kwasababu wewe huachi binti mzuri apite usoni kwako lazima utaingia king. Kinachoendelea ni mawasiliano na baada ya hapo,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, umeliwa!
Kwa upande mwingine wa dada zetu, wanaopenda maisha mazuri bila kuyafanyia kazi. Kuna msemo mmoja unasema “hakuna chakula cha bure- No free lunch”

Marafiki wabaya wanaokunzunguka.
Watu wengi huwa hatupendi kuwaletdown marafiki zetu hivyo wakija na dili lolote hata kabla ya kulifanyia utafiti unajikuta ni sehemu ya kinachofanyika. Katika ulimwengu tuliopo jifunze kuwa mtafiti na kufanya kitu sahihi bila ya hivyo utajikuta ukiangukia matatizo mengi kwa sababu ya marafiki au watu wanaokuzunguka kila siku.

na Bongo 5

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: