Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam
(DAWASCO), imetangaza kuwako na ongezeko la Maji katika maeneo mbalimbali ya
jiji la Dar es salaam, pamoja na maeneo ya miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani
Pwani, baada ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini kuanza kufanya majaribio ya
uzalishaji wa Maji .
Akiongea na waandishi wa habari kaimu meneja
uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa kutokana na ongezeko
hilo la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na pia kumekuwepo
na ongezeko la uvujaji wa Maji katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam,
hasa katika maeneo ambayo yalikuwa na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na
huduma ya Maji na baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo
mdogo (Low pressure)
“Kufuatia
ongezeko hili la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na uvujaji
wa Maji umeongezeka katika maeneo ambayo aidha yalikuwa na miundombinu ya Maji
lakini hayakuwa na huduma ya Maji au maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa
msukumo mdogo” Alisema Bi. Lyaro.
Aidha, ametoa wito kwa wateja na wananchi wote
kutoa taarifa za uvujaji huo wa Maji pindi wanapobaini kuwapo na uvujaji wa
Maji katika makazi yao na maeneo mbalimbali ya jiji kupitia kituo cha huduma
kwa wateja kwa kupiga simu namba 022194800 au 0800110064 (Bure).
“Namba hizi ziko wazi saa 24 kwa siku na mteja
hatakatwa gharama yoyote akipiga simu hizi. Hivyo tunaomba wateja wetu
waisaidie Dawasco kupunguza upotevu wa maji kwa kutupa taarifa za mivujo na
kupasuka kwa mabomba” alisema bi Lyaro.
Kutokana na ongezeko hilo la Maji maeneo
yaliyoanza kupata Maji baada ya majaribio ya mtambo huo kuwa ni Tandale,Manzese
makunimula,Mwananyamala,Kinondoni mkwajuni, baadhi ya maeneo ya
vingunguti,changombe,ubungo-mabibo na city centre.
Pia, DAWASCO imetumia nafasi hiyo kuwakumbusha
wateja wote kulipia huduma ya Maji kwa wakati kwani watu wengi kwa sasa
wameanza kupata huduma ya Majisafi na salama kutokana na kuongezeka kwa
uzalishaji wa Maji katika mtambo wa Maji wa Ruvu chini, hivyo hawana budi
kuyalipia ili kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma ya Maji.
Kuongezeka kwa huduma ya Maji katika jiji la Dar
es salaam na Mji wa Bagamoyo kumetokana na kukamilika upanuzi wa
mtambo wa Ruvu chini ulioanza mwaka 2011 hivyo kuongezeka kiasi cha uzalishaji
wa Maji kutoka wastani wa lita milioni 182 hadi lita 270 kwa sasa.
No comments:
Post a Comment