Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Ijumaa Kuu ni siku ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa. Kadiri ya Mtume Yohane kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka, jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.
Ijumaa kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaani Masiya au Kristo). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi. Ijumaa kuu ni pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake, kulala kaburini, na hatimaye kufufuka kwa utukufu
Siku tatu kuu za Pasaka ndizo kiini cha mwaka wa Kanisa. Zinamuadhimisha Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, yaani siku ya kwanza (Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni) inaadhimisha mateso yake kuanzia karamu ya mwisho hadi kifo cha msalaba; siku ya pili (Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni) inaadhimisha maiti yake kubaki kaburini na roho yake kushukia kuzimu; siku ya tatu (kuanzia Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni) inaadhimisha ufufuko wake mtukufu.
Siku hizo tatu ni kama bawaba kati ya Kwaresima na kipindi cha Pasaka.
Ikiwa leo ni siku ya Ijumaa kuu ambayo wakristo ulimwenguni wanakumbuka mateso ya mkombozi Yesu Kristo takribani miaka 2000 iliyopita, aliacha mbingu na mamlaka ili kuja kunikomboa mimi na wewe na kurudisha uhusiano wetu na Mungu wetu, hakika ni jambo la ajabu ambalo haliwezi kufanywa na mwanadamu awaye yeyote.
No comments:
Post a Comment